Mwakilishi wa Huawei (kushoto) akipokea Tuzo ya Simu yenye Mfumo Bora kwenye Mkutano wa Dunia wa Mawasiliano 2017.
Barcelona, Uhispania, Februari 28,
2017. Huawei kupitia kitengo chake cha Active Antenna Unit (AAU)
imeshinda tuzo ya Simu yenye Mfumo Bora zaidi katika Mkutano wa Wadau wa
Mawasiliano (MWC) 2017.
Tuzo hiyo ilitambua mchango wa
Kampuni ya Huawei katika ubunifu wa teknolojia na mfumo wake mzuri wa
mawasiliano na kuimarisha kituo chake kwa kizazi kijacho. Ukiratibiwa na
GSMA, mkutano huo wa MWC ni miongoni mwa mikutano mikubwa yenye
ushawishi duniani na Taasisi hiyo inayoandaa Tuzo za Global Mobile ni
miongoni mwa tuzo zinazoheshimika katika sekta ya mawasiliano.
Kitengo cha AAU kimelenga
kuanzisha mfumo huo wa mawasiliano ya simu unawezesha kupata huduma ya
redio kutoka vituo mbalimbali. Hiyo ndiyo kizazi kipya cha Huawei
ambacho kimelenga katika kutafuta ufumbuzi kutokana na kutambua umuhimu
wa kusambaza taarifa.
Kitengo hicho cha Huawei ni
mwendelezo wa uvumbuzi kwa ajili ya kufikia mahitaji wa watumiaji wa
mtandao katika maeneo tofauti. Huduma hii itaendelea kuboreshwa taratibu
kadiri mabadiliko ya kimtandao yanavyoendelea.
Mkuu wa Huawei Huduma za Mtandao,
Zhou Yuefeng alisema “Kulingana na maendeleo ya haraka ya MBB, huduma
mpya kama vile VR, HD Video na mtandao wa wirelesss kwa matumizi ya
nyumbani yote hayvyote vimesababisha kuwapo na hitaji kubwa la
kuimaraisha uwezo wa mitandao,
Wakati huohuo, watumiaji
wanahitaji kupunguza gharama za umiliki (TCO). Mfumo wa Huawei wa AAU
ndiyo unaoweza kuwa msaada kwa watumiaji wa huduma a mitandao kuepukana
na changamoto ya kutopata video zenye ubora. Hivi sasa kitengo cha
Huawei cha AAU kimekuwa suluhisho la biashara ambayo inamwezesha mtu
kutazama video kupitia simu yake mfumo uliounganishwa katika nchi zaidi
ya 60 ulimwenguni kote.
Kwa kutumia teknolojia ya 4.5/5G
imeleta mabadiliko kwa kuongeza ufanisi na kutumia antena ya teknolojia
ya kisasa zaidi. Mfumo huo umefanikiwa kuongeza ubora wa matumizi ya
mtandano mara tano zaidi huku pia ikisaidia kupunguza gharama kiasi
fulani na kuimarisha uzoefu kwa watumiaji wake.
Huawei tayari imeshaanza kutumia
mfumo wa FDD na MIMO pia kitengo cha AAU kimeanza kutumia teknolojia
hiyo kwenye kampuni ya mawasiliano ya China Unicom na vilevile
umeshaanza kutumiwa kwa majaribio kwenye simu China na Japan kwenye
mfumo wa simu kibenki.
Mfumo huo wa Huawei unawawezesha
watu kutumia vyema rasilimali zilizopo katika maeneo ya mijini kwa
ajili ya kuona video, kupunguza utegemezi kwenye vyanzo vingine, kuokoa
muda kutokana na upatikanaji wake wa urahisi kwa asilimia 60 na
kupunguza gharama za ujenzi kwa asilimia 40.
Huawei ilianzisha mfumo wa Easy
Macro 2.0 mwaka 2017 ambao unawezesha GSM/UMTS/LTE, ambayo inaweza
kukuwezesha kuona video kwa mlalo au mshazari. Mfumo huo wa Huawei
umekuwa mkombozi kwa kutumika katika mitandao ya kibiashara duniani
ikiondoa kikwazo kilichokuwapo awali katika kupatikana video kwenye
simu.
Mfumo wa Huawei wa multi band
unaosimamiwa na kitengo cha AAU unaweza kuwezesha mpaka bendi 7 pamoja
na 4t4R na kupunguza uwingi wa vifaa na kuandaa video iwapo unahitaji
kukodisha eneo.
Mfumo wa Huawei wa AAU ndio
unaoongoza katika mabadiliko ya matumizi ya mtandao. Kuwapo kwa mfumo
mpya wa 5G hii imerahisisha zaidi na watumiaji kupata video zenye ubora.
Mkutano wa wadau wa mawasiliano
mwaka huu ulifanyika kuaniza Februari 27 hadi Machi 2 jijini Barcelona,
Uhispania. Huawei ilifanya maonyesho ya bidhaa zake za mfumo wa ndani wa
mawasiliano ambazo eneo la 1J50 in Fira Gran Via katika ukumbi 1,
sehemu ya 3130 kwenye ukumbi 3 na Mji wa Ubunifu kwenye ukumbi 4. Kwa
maelezo zaidi tafadhari tembelea kwenye tovuti yetu.
Tags
BIASHARA