Rapper Nay wa Mitego, Alhamis hii aliitikia wito wa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kukutana naye mjini
Dodoma kwaajili ya kuzungumza namna ya kuuboresha wimbo wake Wapo ambao
licha ya kuikosoa vikali serikali pamoja na Rais Dkt John Magufuli
umepokelewa kwa mikono miwili.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Rais Magufuli kuamuru kuachiwa huru kwa Nay
ambaye alikuwa amekamatwa na polisi na wimbo wake kufungiwa na BASATA.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Dkt Mwakyembe alisema
wasanii wana nafasi kubwa katika kuisaidia serikali kukemea mambo maovu.
Amewataka vijana kutambua kuwa Tanzania ni nchi inayozingatia utawala wa
sheria na kwamba wana uhuru wa kukosoa bila kutukana au kwenda nje ya
maadili. “Na ndio maana tukasema kwa wimbo wa Nay hapana, hebu ngoja
tuusikie, mbona ni wimbo mzuri tu,” alisema Mwakyembe.
Tags
Nay wa Mitego
