Staa wa utotoni, Hanifa Daudi maarufu kama Jennifer kwenye filamu za
marehemu Steven Kanumba, amedai kuwa siku za mwanzo wakati ameingia
kidato cha kwanza, walimu na wanafunzi walikuwa wakimuogopa wakidhani ni
mchawi kweli.
Kwenye moja ya filamu za Kanumba, Hanifa aliigiza kama mchawi.
“Vituko vilianza nilipoanza form one nikachukuliwa nikapelekwa boarding
iko Same sasa kunipata shida watu walikuwa wananijaalia,” Hanifa
alikiambia kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM kinachoendeshwa na
Raheem Da Prince.
“Kuanzia walimu hadi wanafunzi walikuwa wananiona mtu wa ajabu labda
ntakuwa naringa, mpaka wengine wakawa hawaamini, wanasema naweza nikawa
mchawi kweli wakawa wananitenga,” alisema.
“Lakini baadaye sikufanikiwa kuhama nilimaliza pale form four watu walinizoea,” aliongeza.
Hanifa amemaliza kidato cha nne mwaka jana na alipata division two ya 21.
Kwa upande wa mama yake mzazi ambaye anaamini filamu za Kibongo zimekufa
tangu kifo cha Kanumba, amesema mwanae yupo wazi kwa atakayetaka
kumsimamia kwenye masuala ya filamu ila makubaliano yao yatamhusisha
mwanasheria.
Tags
KIBURUDANI
