Mrembo mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha mpango
maalum wa kufundisha somo la ujasiriamali kwa wanafunzi wa kidato cha
pili wa shule ya sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti katika
Manispaa ya Ilala.
Jokate ataanza mafunzo hayo maalum kwa wanafunzi wa kike kuanzia wiki
ijayo na lengo la mafunzo hayo ni kuwapa ufahamu wanafunzi hao na
kuanzisha biashara zao mara baada ya kumaliza elimu yao ya sekondari.
Alisema kuwa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi ni muhimu kwani
yanawawezesha kujiandaa vizuri kukabiliana na maisha mara baada ya
kuhitimu masomo yao ya sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya
ngazi ya juu.Kwa mujibu wa Jokate, unaweza kusoma mpaka Chuo Kikuu ndani
na nje ya nchi, lakini bado utakabiliana na ugumu wa kupata ajira
ambazo kwa sasa ni haba.
“Kuna wengine wamesomea taaluma fulani kwa ngazi ya Chuo Kikuu lakini
mpaka sasa hawana ajira na kukata tama katika maisha, pia unaweza
kufanya kazi tofauti na taaluma uliyosomea, lakini kwa ujasiriamali ni
tofauti, utajifunzi jinsi ya kupata mtaji, kukopa na kurejesha, kufanya
biashara gani na mbinu zake,”
Tags
ELIMU

