Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo amejibu swali la
waandishi kadhaa wa habari waliomhoji mapema leo baada ya kuapishwa
katika viunga vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mwakyembe amenukuliwa akisema maneno yafuatayo juu ya sakata hilo
lililotikisha vichwa vya habari nchini kwa juma moja sasa.
"Ninachokijua kuhusu tukio la Clouds Media kinatokana na vyombo vya
habari, sidhani kama taarifa hizo zinatosha mimi kutoa uamuzi"-Waziri
Mwakyembe
Tags
MWAKYEMBE
