Aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi Shy-Rose Bhanji amelalamika jina lake kukatwa katika
kinyang'anyiro cha kutetea nafasi hiyo katika muhula ujao bila kuhojiwa
juu ya tuhuma zilizopeleka jina lake kukatwa.
Licha ya malalamiko hayo, pia Shy-Rose Bhanji ametumia fursa hiyo
kuwapongeza watu waliochaguliwa kuwa wagombea wa Bunge la Afrika
Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuwashukuru wabunge
kwa kumpigia kura zilizomuwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa
mwanzo waliopata kura nyingi zaidi.
"Ingawa jina langu limekatwa na Kamati Kuu ya Chama bila ya mimi nwenyewe kuitwa na kuhojiwa ili nipewe haki ya kujibu hoja zozote dhidi yangu, nawapongeza wote waliochaguliwa kuwa wagombea wa EALA kupitia CCM. Ninawashukuru sana Wabunge kwa kunipigia kura nyingi zilizoniwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo walioongoza kwa kura" aliandika Shy-Rose Bhanji
