Frank Lampard ambaye ni moja ya viungo waliocheza kwa mafanikio kwenye
klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Uingereza, amesema kuwa kiungo Paul
Pogba bado hajaishi matarajio ya wengi yaliyopelekea klabu ya
Manchester United kulipa fedha zilizovunja rekodi ya usajili duniani, na
amesema kuwa mchezaji huyo anaweza kuja kuwa “tatizo la paundi milioni
90” ndani ya Old Trafford.
United walilipa kiasi cha takribani paundi milioni 89.3 (£89.3m) kumleta Pogba ndani ya Old Trafford kutokea Juventus mwezi Agosti, na ameendelea kucheza vyema chini ya kocha Jose Mourinho lakini pia amejikuta katika wakati mgumu na siku za karibuni tangu mechi ya fainali kati ya Southampton dhidi ya Manchester United.
Pogba amefunga mara 4 tu kwenye michezo 25 ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu na hii imemfanya Lampard ni wazi kuwa bado Manchester United inategemea makubwa zaidi kutoka kwa mchezaji huyu hasa kutokana na uwekezaji uliowekwa kwake.
“Hii ndio ishara ya wao kuwekeza kiasi cha £90m ambaye binafsi ningesema ni ambaye bado hakuwa mtimilifu na ana nafasi ya kukua zaidi,” alisema Lampard. “Ina vitu vingi ndani yake vya msingi. Ana nguvu, ana miguu yenye ubora, ana mwili mkubwa kuliko wewe na ni mwepesi kuliko wewe kwenye eneo la kiungo.
“Lakini ukishakuwa na kiasi cha paundi milioni 90 (£90m) mabegani kwako, tunachambua zaidi na tunahitaji zaidi. Bado najiuliza nafasi yake bora ni ipi. Ni mchezaji wa aina gani na anataka kuwa mchezaji wa aina ipi?
“Nahisi ameanguka na hajafanikiwa karibia katika kila kitu. Unapoamua kulipa £90m unahitaji kuona matokeo, na hajazalisha matokeo yaliyotarajiwa. Ni mdogo bado na pengine anaweza kufanikiwa, lakini kwa hali ilivyo mpaka sasa bado hajawa mchezaji wa kubadili mchezo.”

Tags
MICHEZO KIMATAIFA