Waraka wa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema kuachiwa juma
lijalo. Waraka huo, niliopata bahati ya kuuchungulia, unabeba mambo
muhimu yahusuyo hasa haki za binaadamu. Mambo hayo yalionwa na kusikiwa
na Lema alipokuwa Mahabusu Kisongo kwa takribani miezi minne.
Waraka huo maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na
viongozi wengine,unaibua pia njama mbalimbali zinazofanywa na
wakandamizaji wa haki za binaadamu. Lema pia anaanika simulizi zenye
kuliza za mahabusu wanaopigwa danadana kwenye kesi zao na kuwafanya
wasitendewe haki.
Lema ameandika. Lema anataka Rais ajue. Anataka ujumbe umfikie Rais na
marekebisho yafanyike. Lema ameapa kuendelea kusema ukweli na kuusimamia
kwa namna yoyote iwezekanayo. Lema hatanii, anasema na kufanya kweli.
Kaeni mkao wa kula kwa Waraka huo wa Mbunge Lema kwenda kwa Rais.
Tags
SIASA
