Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
ameachiwa kwa dhamana (ya polisi) iliyowekwa na wanasheria wawili,
Hekima Mwasipu na Nashon Nkungu baada ya kushikiliwa na polisi kwa saa
kadhaa .
Lissu alikamatwa ghafla jana alipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu baada ya mashitaka yake ya uchochezo katika moja ya kesi
zinazomkabili, kufutwa.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lissu
alikamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi ambayo
yangeweza kuibua mtafaruku wa kidini katika jamii wakati alipokuwa
akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Dimani,
Zanzibar, mwezi Januari mwaka huu.
Baada ya mahojiano ya jana, Lissu ameachiwa kwa sharti la kuripoti Kituo
Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Machi 13, mwaka huu.
Tags
SIASA
