TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA USTAWI WA JAMII DUNIANI (WORLD SOCIAL WORK DAY) TAREHE 21 MACHI 2017
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Chama Cha Wanataaluma
ya Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) inautaarifu umma kuwa itaungana na
wataalam wa ustawi wa jamii duniani kote kuadhimisha Siku ya Ustawi wa
Jamii Duniani mnamo tarehe 21/03/ 2017 katika viwanja vya Taasisi ya
Ustawi wa Jamii iliyoko Kijitonyama, jijini Dar es Salaam kuanzia saa
3.00 asubuhi.
Maadhimisho yatatanguliwa na
matembezi ya amani yenye kusisitiza umma juu ya majukumu, wajibu na
mchango wa taaluma ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla. Matembezi
hayo yataanzia katika kituo cha mabasi cha ITV kilichopo eneo la mwenge.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Mb) Mheshimiwa Dkt. Hamis
A. Kigwangala.
Kauli mbiu ya siku hii kwa mwaka 2017 inasema “USTAWI WA JAMII: KUKUZA NA KUIMARISHA JAMII NA MAZINGIRA”.
Katika kuadhimisha siku hii huduma
za ushauri nasaha, ushauri na upimaji wa Virusi vya UKIMWI, upimaji wa
magonjwa ya moyo na huduma nyingine zinazohusiana na matatizo mbalimbali
ya kijamii vitatolewa bure. Hivyo, wote mnakaribishwa.
Ili kufikia azma ya serikali ya
kuwa nchi ya viwanda, tunahitaji jamii zilizo bora na mazingira rafiki
kwa kila mtu hivyo tunatoa rai kwa kila mtanzania kulinda mazingira
yanayomzunguka.
Erasto Ching’oro
Msemaji – Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Tags
HABARI KITAIFA