Ikiwa tunaelekea kwenye wekeend yaani Jumamosi na Jumapili ambapo watu
wengi hupata nafasi ya kupumzika na kufanya mambo yao binafsi.
Wapo ambao hutumia siku za weekend kwa kutulia nyumbani tu, huku wakijiandaa na kujipanga vyema ili kuanza wiki ijayo vizuri.
Siku kama ya kesho yaani Jumamosi itapendeza kama ukiitumi kwa kukamirisha kazi zako muhimu hasa zile za nyumbani.
1. Tumia weekend yako kufanya usafi kwa ujumla
Inawezekekana ikawa ni usafi wa kufua nguo, kusafisha nyumba, vyombo
pamoja na kufagia, ni vyema ukajitahidi siku za weekend ukawa unafanya
usafi wa kutosha na wakuridhisha kabisa kwasababu mara nyingi katikati
ya wiki huwa ni ngumu kupata muda wa kuyafanya hayo tena.
2. Tumia weekend yako pia kukamirisha zile kazi zako ambazo ulishindwa kuzikamirisha katikati ya wiki.
3. Ikiwa mambo yako yote muhimu na ya lazima uliyakamirisha katikati ya
wiki na yote yapo sawa, basi weekend yako itumie kwa kufanya mambo mapya
unayopendelea kufanya au kujifunza. Mfano kupika, kuogelea n.k
4. Kwa wanafunzi wao ni vyema wakatumia wikeend zao kumalizia kazi za shuleni kama ni homework / assignments.
5. Pia hakikisha unatumia weekend yako kwa kupanga ratiba yako yote
utakayofanya juma lijalo. Panga kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa utafanya
nini, huku ukizingatia muda maalum wa kufanya mambo hayo.
6. Ukiwa na nafasi pia unaweza kuwakumbuka watu wako wa karibu kama
ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwatembelea au kuwasiliana nao. Weekend
hii kama una nafasi waoneshe ndugu, jamaa na marafiki kuwa unawajali na
kuwapenda kwa kuwatembelea au hata kuwatumia salamu kwa njia ya SMS na
kuwapigia simu.
