Wogeleaji wakishindana katika mashindano yaliyopita ya kuogelea.
Peter Itatiro ‘akikata’ maji katika mashindano yaliyopita ya kuogelea.
…………..
Na Mwandishi Wetu
Mashindano
ya kutafuta bingwa wa Taifa wa mchezo wa kuogelea yamepangwa kufanyika
Aprili 7 na 8 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Heaven of Peace
Academy (Hopac) iliyopo Kunduchi Mtongani.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya timu 19 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na visiwani.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alizitaja
timu ambazo zinatarajia kushiriki kuwa ni Dar es Salaam Swimming Club,
Taliss swimming club, Bluefins, JKT, Morogoro International School,
Champions Rise, Braeburn International School na shule ya sekondari ya
Makongo.
Timu
nyingine ni ISM Leopards, Arusha Swim Club, Mwanza Swim Club, Kennedy
School Arusha, Stingrays Swim Club, Tanzania Marines, Hopac Swim Club,
Genesis Swim Club, KMKM, Wahoo –IZS na Zanzibar Dolphins.
Waogeleaji
hao watashinda katika stali nne ambazo ni freestyle, backstroke,
Individual Medley na breaststroke. Pia kutakuwa na mashindano ya ‘relay’
ambayo yatashirikisha waogeleaji wa kike na wa kiume.
“Tunatarajia
kuwa na mashindano myenye ushindani mkubwa kutokana na maandalizi ya
kila timu, mchezo unakuwa na timu zinazidi kuongezeka, kwa kifupi kuna
mwamko mkubwa sana katika mchezo, tunawaomba wadhamini wajitokeze
kutusaidia,” alisema Namkoveka.
Alisema
kuwa kwa sasa wapo katika maandalizi ya kuhakikisha mashindano hayo
yanafanyika kwa kiwango cha kimataifa na kwa kutumia sheria za
shirikisho la mchezo huo duniani, Fina.
“Mashindano yatakuwa ya umri, kutakuwa na umri kati ya miaka 9 -10, 11-12, 13-14, 15-16 ba
zaidi ya 17, hakuna muogeleaji atakayeruhusiwa kushiriki katika
shindano zaidi ya moja, viongozi wote wa timu watanakiwa kufika kwenye
mkutano utakaofanyika Hopac kabla ya mashindano kuanza, mkutano huo
utaendeshwa na kamati ya ufundi,” alisema.
Tags
KUOGELEA