Mjasiliamali Nafue Nyange akisisitiza jambo.
Miss Tanzania 2014, Nargis Mohamed.
Mjasiliamali Nafue Nyange.
Miss Tanzania 2014, Nargis Mohamed na Nafue Nyange wameamua kufungua shule ya urembo watakayokuwa wakiitoa kwa njia ya mtandao.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam
na waandishi wa habari Nargis alisema kuwa wameamua kuandaa mafunzo hayo
maalum katika fani ya urembo ili kuweza kuwawezesha wananwake na vijana
waweze kujikwamua kiuchumi.
Nargis aliongeza kuwa mafunzo hayo
maalum yamewalenga watu wote na wanaweza kuyapata kidigitali zaidi
ikiwemo njia ya simu au mtandao kwa gharama ya shilingi elfu kumi
(10,000) tu za kitanzania kwa mwezi.
“Mafunzo hayo hayachagui jinsia;
nia yetu kubwa sisi ni kuwawezesha wenzetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze
kujiinua kiuchumi kama wajasiliamali na kujijenga kimaisha sambamba na
mpango wa serikali yetu kujenga ajira na kujikwamua kutoka kwenye
umaskini,” alisema Nargis.
Kwa upande wake Nafue Nyange
aliongeza kuwa mafunzo hayo yanapatikana kwa bei nafuu kabisa kupitia
tovuti ya www.glammadamlive.com, anawaomba watanzania wasajili wataweza
kufanya malipo kupitia Vodacom M-pesa na Tigo Pesa. Kwa wale walio nje
ya nchi wanaweza kutumia kadi tofauti kama VISA,MasterCard,American
Express.
Tags
UREMBO