Kamanda wa polisi mkoani
Pwani,Onesmo Lyanga akizungumza jambo na wananchi wa kitongoji cha
Mpalange,kijiji cha Ikwiriri Kaskazini,kuhusiana na masuala ya ulinzi na
usalama kwa raia.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,akizungumza
na wananchi nje ya kituo cha afya cha Mchukwi baada ya kwenda
kumtembelea mwenyekiti wa kitongoji cha Mpalange,Bakari Mpawane
aliyejeruhiwa kwa kupigwa risas.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi
Evarist Ndikilo,ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
mkoani hapo,akimfariji mwenyekiti wa kitongoji cha Mpalange huko,Bakari
Mpawane ambae amepigwa risasi na watu wasiojulikana
Mkuu wa mkoa
wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo,ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama mkoani hapo,akiingia katika kituo cha afya cha
Mchukwi,wilaya ya Rufiji kwenda kumtembelea na kumpa pole, mwenyekiti wa
kitongoji cha Mpalange ,Bakari Mpawane ambae amepigwa risasi na watu
wasiojulikana.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
Mwenyeki
kitongoji cha Mpalange ,kijiji Ikwiriri Kaskazini,wilayani Rufiji
mkoani Pwani ,Bakari Mohammed Mpawane ,amenusurika kifo baada ya kupigwa
risasi na watu wasiojulikana.
Tukio
hilo ni tatu kutokea ndani ya mwezi mmoja uliopita likihusisha kupigwa
risasi na kuuawa wenyeviti wa vitongoji na vijiji katika hali ya
sintofahamu.
Kufuatia
matukio hayo kukua kwa kasi,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,ametangaza mapambano na mtandao wa
wahalifu wanaofanya matukio mbalimbali ya mauaji wa kutumia silaha na
kuweka hofu kwa jamii.
Mbali
na hilo ,aliweka bayana kuwa,inspector jeneral wa polisi (IGP)Enerst
Mangu ametangaza dau la mil.tano ,kwa mtu yeyote atakayemtaja ama kutoa
taarifa ya kundi la wahalifu wanaohusika kufanya matukio hayo .
Akizungumza
mara baada ya kwenda kumtembelea mwenyekiti huyo katika kituo cha afya
Mchukwi anapopatiwa matibabu,mhandisi Ndikilo,alieleza kuwa tukio hilo
limetokea march 19 majira ya saa mbili usiku wakati akiwa kwenye duka
lake .
Alisema
walifika watu wawili dukani hapo wakiwa kwenye pikipiki ambapo mmoja
alimwita jina mwenyekiti na kabla ya kutaharuki alijikuta akipigwa
risasi mbili ya mkononi na tumboni na mtu mwingine aliyepakiwa nyuma ya
pikipiki hiyo.
Mhandisi Ndikilo,alibainisha kwamba,bahati nzuri risasi hizo zilipalaza hivyo hazikumuathiri na kuokoka maisha yake.
“Ni tukio la tatu kwa mwezi mmoja likiwemo lililotokea machi 13 mwaka huu mwenyekiti
wa kitongoji cha Kazamoyo wilayani hapa, Hemed Njiwa (45) ameuawa kwa
kupigwa risasi akiwa nyumbani na lile tukio lililohusisha kifo cha OC
CID”alisema .
Hata hivyo mhandisi Ndikilo,alieleza wanaendelea kuwasaka watu hao usiku na mchana hadi kuhakikisha wanawakamata watu hao.
“Tutawasaka
na hatafanikiwa kwa mipango yao waliojiwekea tumejidhatiti na
tutahakikisha tunategua mipango yao na kurejesha amani kwa
wananchi”alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi
Ndikilo ,alishukuru wahudumu wa afya katika kituo cha afya cha Mchukwi
kwa kuokoa maisha ya mwenyekiti bkari pamoja na kutoa huduma nzuri kwa
majeruhi na wagonjwa wengine wanaofikishwa hapo kupata matibabu.
Kwa
upande wake,kamanda wa polisi mkoani Pwani,Onesmo Lyanga,alitaja mtandao
wa watu zaidi ya 100 wanaoshukiwa kuhusiaka na matukio ya kiuhalifu
kuanzia eneo la Mkuranga-Utete-Kibiti-Rufiji hadi Bungu .
Alisema
majina wanayo na wanayafanyia kazi hivyo wanaomba ushirikiano wa
wananchi kutoa taarifa polisi mara wanapopata wasiwasi wa watu
wanaoingia kwenye maeneo yao.
Kamanda
Lyanga,alisema ameletwa mkoa wa Pwani kutoka Simiyu,kikubwa anahitaji
ushirikiano na jamii ili hali kupunguza matukio yanayotikisa ikiwemo la
kuuwa wa wenyeviti wa vitongoji,watendaji na wenyeviti wa vijiji.
Nae majeruhi mwenyekiti wa kitongoji cha Mpalange,Bakari alisema anashukuru mungu ni mkubwa anaendelea vizuri.
Alisema
wanaishi katika hali ya hofu na anajifikiria endapo akirudi kwake baada
ya matibabu ataishije wakati akiwa katoka kwenye tukio kubwa na la
uuaji kama hilo.
“Naomba
serikali na jeshi la polisi liweke mikakati kabambe ili kuvunja ngome
za kiuhalifu na mtandao unaomaliza hasa viongozi bila kujua chanzo ni
masuala ya kisiasa ama nini”alisema
Tags
USALAMA