Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya
kutembelea Bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya
udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la
Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari, kuhakikisha ukaguzi
wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo
humaliza nguvu kazi ya Taifa. Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya
Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitembea kuelekea sehemu
inayokaguliwa mizigo wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar,
ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za
Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar, kushirikiana na
Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili
kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya
Taifa.Wakwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum na
anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu
Abdula Juma.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua jinsi ukaguzi wa mizigo
unavyofanyika kupitia komputa wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya
Zanzibar ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa
Dawa za Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana
na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili
kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.
Kulia ni Afisa wa Bandari anayeshughulika na ukaguzi, Adam Masoud.
Mfanyakazi wa kitengo cha mizigo
Bandari ya Zanzibar, Saleh Masoud akikagua moja ya mzigo wa abiria
wanaoingia kupitia bandari hiyo ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,ameliagiza Jeshi la Polisi
Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari hiyo kuhakikisha ukaguzi wa
mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa Dawa za Kulevya ambazo
zimekuwa zikiharibu nguvu kazi ya Taifa.
Mkurugenzi Mkuu Bandari ya
Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma (wapili kushoto), akimsikiliza
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
wakati wa ziara ya kutembelea bandari hiyo ikiwa na lengo la kukagua
mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza
Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi
wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza
nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed
Ahmada Salum na wakwanza kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
Johari Masoud Sururu.
Kifaa cha kubebea kontena kikiwa
kimebeba kontena tayari kupelekwa kwenye mashine maalumu ya ukaguzi
ambayo hutumia mionzi kukagua mzigo uliopo ndani, ambapo Naibu Waziri
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza
Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari ya Zanzibar kukagua
mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya
Visiwani Zanzibar.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Tags
BIASHARA HARAMU