Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye
kupitia ukurasa wake wa twitter amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia
busara kumwachia msanii Nay wa mitego huku akienda mbali na kudai kuwa
matumizi ya nguvu kubwa hayana faida yoyote.
“Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera
Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!"
Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia juzi ambapo alipelekwa katika
Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi
cha Kati jijini Dar es Salaam.Alikuwa anatuhumiwa kwa kutoa wimbo ambao
unaikashifu serikali.
Hata hivyo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, jana mchana alitoa agizo kwa Jeshi
la Polisi kumuchia huru msanii huyo na kutaka wimbo wake ‘Wapo’
uendelee kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali,
Tags
Nape Nnauye
