Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana imesikiliza malalamiko ya
watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri
lililofunguliwa mwaka 2014.
Wakizungumza mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa jana ndiyo
itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande
wa jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao.
Wamesema wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia
zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa
makosa ya kusingiziwa.
Aidha wamesema wamekuwa wakipewa ahadi hewa na mkuu wa upelelezi kuwa
angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la
mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba linaleta ukakasi
kwa wananchi.
Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa
na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April
11 mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati
akifanya utaratibu wa kumtafuta mkuu wa upelelezi na kuzungumza naye
