Rais wetu kipenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, jana alifanya yale ambayo huwa anayapatia kweli kweli!!
Kwa kutumia umahiri mkubwa kabisa, bila shaka aki-apply mbinu za kijeshi
alizowahi kujifunza JKT, Mheshimiwa Magufuli aliingia bandarini kwa
kushitukiza hali iliyowafanya watu wa pale wapigwe butwaa huku wengine
mioyo yao ikipiga mkamba kwa sababu hawakutarajia kutokea Mheshimiwa
huyo!!!
Mbinu hizi za kijeshi, na bila shaka zikichanganyika na mbinu za
kijasusi; zilimwezesha Mheshimiwa Rais wetu aweze kukamata makontena
kadhaa yaliyojaa dhahabu!!!
Huku akionekana kujawa na uchungu kwa nchi yake, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alisema:
Kwa taarifa nilizonazo, nikizisema hapa mnaweza mkalia! Dhahabu iliyopo humu ndani! Kwa Mtanzania yeyote anayeipenda Tanzania... atalia! Kwa mali zilizomo humu...!
Tags
RAIS MAGUFULI
