Mechi mbili za kwanza hatua ya
Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (Azam Sports Sports Federation
Cup 2016/2017), zitachezwa Machi 18, mwaka huu kwenye viwanja viwili
tofauti.
Mechi hizo ni kati ya Kagera
Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini
Bukoba mkoani Kagera kadhalika Simba itakayosafiri hadi Arusha kucheza
na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mechi nyingine zitapangiwa tarehe
za baadaye. Mechi hizo ni kati ya Azam FC na Ndanda FC kadhalika
Tanzania Prisons ya Mbeya itakayocheza na mshindi kati ya Young Africans
ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni.
Pia bingwa wa michuano hiyo,
ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho
Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye
ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tags
MICHEZO KITAIFA