Jana kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi
alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili Saida Karoli ambapo alikiri kuwa
hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na
Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai
zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye
haki nazo.
Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond
Platnumz aliurudia ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani
hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea.
”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo,
sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio
alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi
maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa
bure
”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja
“Meneja wa zamani aliniuliza nyimbo yako inatakiwa kutumika lakini nipe
idhini yako japo ni nyimbo zangu zote lakini sikuwa na haki licha ya
kuwa sauti yangu imesikika kule, mimi nilimjibu nimeshakata tamaa na
kuimba naona muziki kwangu hauna faida na thamani bora kuwa hata mkaanga
vitumbua au maandazi kuliko kuimba
”Nilikuwa na mpango wa kurudi kijijini nyumbani nikae mtu akihitaji show
atanikuta kijijini lakini meneja akanambia hapana, alisema nyimbo tumpe
Diamond kwa sababu itaniinua na kunipa moyo na kuniamsha upya kama mtu
aliyekufa
“Walizushaga nimekufa na nilihisigi nimekufa kweli kutokana na hali ya
maisha na nilikuwa nimekata tamaa nikajua nimekufa kweli” Alisema Saida
Karoli
Kwa sasa Saida yupo Dar na amekuja rasmi kwa ajili ya kufanya muziki
upya kama zamani na yupo tayari kufanya kolabo na wasanii kama Ben pol,
Bell 9, Diamond na Darassa.
Tags
ELIMU
