Baada ya kufunga magoli mawili
katika michuano ya Europa League dhidi ya ndugu zao KAA Gent
Mshambuliaji na Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta huku KRC Genk
wakishinda jumla ya magoli 5-2 na kuandikwa na vyombo mbalimbali barani
Ulaya hatimaye Leo ameifungia timu yake bao katika ushindi wa magoli 4-0
dhidi ya KVC Westerlo kwenye dimba la Het Kuipje.
Ilichukua dakika ya 7 Mbwana
Samatta akifunga goli la uongozi katika timu yake na mnamo dakika ya
27,Thomas Buffel hadi mapumziko wageni walikuwa mbele kwa 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote mbili kufanya mabadiliko hata hivyo wageni waliweza kunufaika
kwani kunako dakika ya Omar Colley alifunga dakika ya 62 na dakika ya
90,Malinovsky akipingilia msumari wa nne ukiwa mchezo wa kufunga Ligi
kuu ya Ubelgiji huku Genk wakifikisha jumla ya pointi 48 kwenye nafasi
ya nne ya Msimamo.
Hadi mwamuzi akipuliza kipyenga
cha mwisho Genk wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 4-0 huku Samatta
akifikisha jumla ya magoli 10.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA