Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya
Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’,
kesho Jumamosi tarehe 04 Machi, 2017, watatembelea Kituo cha vijana
wanaopatiwa matibabu baada ya kuathirika na dawa za kulevya.
Kituo hicho kinachoitwa Sober
House kipo Bagamoyo mkoani Pwani. Ni kituo maalumu kwa tiba ya vijana
kinaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Life and Hope Rehabilitation
Centre chini ya Mkurugenzi, Al-Karim Bhanji.
Ikiwa huko, vijana wa Serengeti
Boys ambao kwa sasa wako kwenye kipindi cha mabadiliko ya katika sayansi
ya mwili hivyo itakuwa somo kubwa kwao katika kujielimisha kuhusu
mustakabali wa maisha yao.
Kwa upande wa TFF kuwapeleka
vijana hao huko ni utekelezaji Kanuni ya 36 (7) ya Ligi Kuu ya Vodacom
inayozungumza kukataa rushwa, madawa, ubaguzi, fujo, kamari na mambo
mengine ya hatari kwa mchezo wa mpira wa miguu
Tags
MICHEZO KITAIFA