Shehena kubwa ya pombe haramu iliyofungashwa kwenye mifuko aina ya
viroba kutoka nchi ya uganda kwa njia za magendo imekamatwa ikiwa
imehifadhiwa kwenye gari lililojengwa nje ya mji kata ya Nshamba wilaya
ya Muleba mkoa wa Kagera huku kiwanda cha kuzalisha pombe kali
inayosadikiwa haifai kwa matumizi ya binadamu kimefungiwa.
Kukamatwa kwa ghala lililosheheni pombe kali kutoka nchi jirani ya
Uganda na kufungwa kwa kiwanda cha pombe kali ni matokeo ya operesheni
inayohusisha jeshi la wananchi, uhamiaji,magereza,polisi na mgambo kwa
lengo la kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na pombe haramu hapa
nchini ambapo operesheni hiyo imefanikiwa kuwakama ta watuhumi wa watatu
wakiwa na katoni 800 za viroba na tani nane za kahawa ikisafilishwa kwa
njia za magendo nje ya nchi kinyume cha sheria.
Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Modest Lwakahemula amebainisha madhara ya kutumia pombe kali.
Baadhi ya wananchi wameipongeza serikali kuanzisha operesheni ya
kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na pombe kali hapa nchini.
Tags
POMBE ZA VIROBA
