| Mhe. Waziri
Mahiga akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa timu ya mpira ya
Everton ya nchini Uingereza. Timu hiyo ipo katika hatua za mwisho za
maandalizi ya kuja Tanzania kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki. Mhe.
Waziri alisema ziara hiyo itasaidia kuitangaza Tanzania duniani pamoja
na kuhamasisha mchezo wa mpira wa miguu kwa vijana wa Kitanzania.
Anaozungumza nao kutoka kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Mpira wa Miguu
(Head of Football Operations) wa timu hiyo, Bw. David Harrison; Mkuu wa
Ulinzi na Usalama (Head of Safety and Security) wa timu, Bw. Dave Lewis
na Bw. Alan Chisholm kutoka Thomas Cook. |