Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Lissu aliachiwa leo asubuhi na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shahidi baada
ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul Kadushi kuwasilisha hati
ya kuondoa shtaka hilo.
Kadushi aliwasilisha hati hiyo chini ya kifungua namba91 (1) cha makosa
ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi, mahakama
ikaridhia na kumuachia.
Muda mfupi baada ya kuachiwa na kutoka nje ya mahakama alikamatwa tena
na askari waliokuwapo mahakamani hapo na kupelekwa Kituo Kikuu cha
Polisi.
Tags
SIASA
