Hatari! Mama mzazi wa muigizaji mkubwa wa filamu Tanzania, Wema Sepetu,
Miriam Sepetu anadaiwa kuitikisa ndoa ya mfanyabiashara maarufu nchini,
Alex Msama, Risasi Mchanganyiko limepewa mchongo mzima.
ANA KWA ANA NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na ishu
hiyo, mtikisiko huo mkubwa ulitokea ndani ya familia ya muandaaji huyo
wa matamasha ya Injili baada ya mkewe kukuta ujumbe mfupi wa maneno
katika simu ya mumewe, hivyo kusababisha mtafaruku.
“Sijui hasa nini kilitokea, lakini nilicho na uhakika nacho ni kuwa ndoa
ya wawili hao ilikuwa katika majaribu makubwa wakati huo, maana
kulionekana kuwepo kwa mawasiliano ya mara kwa mara baina ya Msama na
Mama Wema, kitu ambacho mkewe alishindwa kuelewa. “Msama alijitahidi
sana kupooza mambo kwa kujaribu kumuweka sawa mkewe, lakini bado ikawa
ngumu hadi baadhi ya marafiki wa karibu wa pande
WAANDISHI WETU, RISASI zote mbili walipoingilia kati na kuliweka sawa
jambo hilo na hivyo kupoa,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilisema
wakati mmoja katika mtafaruku huo, wanandoa hao walikuwa hawazungumzi,
kitu ambacho kilitishia sana uhai wa ndoa hiyo. Baada ya kupata taarifa
hizo, Risasi Mchanganyiko lilifanya juhudi kubwa za kuwatafuta wawili
hao, likifika ofisini na nyumbani kwa nyakati tofauti lakini mara zote
likiambulia patupu. Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Msama
alipatikana kupitia simu yake ya mkononi.
HUYU HAPA ALEX MSAMA
“Ni kweli, ndoa yangu ilipata mtikisiko mkubwa sana kwa sababu ya Mama
Wema, mke wangu alikuta mawasiliano baina yangu na yule mama kwenye
simu, akaja juu. Alikuwa akiniuliza huyu ni nani na kwa nini nawasiliana
naye mara kwa mara.
“Nilikuwa nawasiliana naye mara kwa mara kwa sababu nilikuwa na biashara
naye. Unajua kuna kipindi nilitaka kununua nyumba yake, nikawa wakati
mwingine ninampa hela kidogokidogo, sasa katika biashara kubwa kama ile
ni lazima mtakuwa mnawasiliana mara kwa mara.
“Mke wangu alipokuwa anaona meseji nyingi kutoka kwake, akawa anahisi
kuna kitu, lakini nilijitahidi kumweleza kuwa ni kwa sababu ya biashara
tu, hatimaye alinielewa, mambo yakaisha na sasa kila kitu kiko vizuri,”
alisema Msama. Mke wa Msama ni mtangazaji wa kituo kimoja cha Redio,
kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
VIPI KUHUSU PESA ZAKE?
Risasi Mchanganyiko lilimuuliza Msama hatima ya fedha zake za maudhiano
ya nyumba ambazo hivi karibuni alilazimika kutumia Polisi ili kumkamata,
baada ya kudai kuwa mama huyo alichukua fedha, lakini badala yake
akamuuzia mtu mwingine.
“Hapa ni lazima niwe mkweli, siwezi kukubali huyu mama achukue tu fedha
zangu kirahisi atoweke, ninasikia faili lake tayari limeshafika kwa
Mwendesha Mashtaka wa serikali, ninachotaka mimi ni vyombo vya sheria
kufanya kazi yake ili haki itendeke.
“Sitakubali mazungumzo, maana watu kama hawa wapo wengi sana hapa mjini,
wanafanya mambo makusudi, wakitegemea huruma, siwezi kuwa na huruma na
mtu ambaye anadhani udanganyifu ni jambo zuri, suala hilo ninataka
limalizike mahakamani,” alisema Msama ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni
ya Habari ya Msama Media Group.
MSAKO WA MAMA WEMA
Mbio za kumsaka Mama Wema zilishika kasi na kulifikisha Risasi
Mchanganyiko hadi nyumbani kwake, Sinza Mori, lakini msichana
aliyefungua mlango alisema mwanamama huyo, aliyegonga vichwa vya habari
wiki chache zilizopita kufuatia sakata lake na Steve Nyerere, hakuhitaji
kuonana na mtu yeyote kwa wakati huo.
Kuona hivyo, waandishi wetu walimtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia
simu yake ya mkononi, lakini licha ya kuonyesha kuwa ujumbe huo ulifika
na kusomwa, hakurudisha majibu.
TUJIKUMBUSHE
Alex Msama na Miriam Sepetu wamejikuta wakiingia katika mtafaruku baada
ya kushindwa kuelewana katika suala lao la mauziano ya nyumba ya mama
huyo iliyopo Sinza Lion.
Tags
MAMA WEMA
