1.Kuna chakula/tunda unalolipenda zaidi? Jiwekee zawadi, kwamba ukiamka
asubuhi tu cha kwanza ni kula chakula hicho/ tunda/ chokleti nk. Hii
itakufanya Utoke kitandani pale tu utakaposhtuka!
2.Iwekee Kipaumbele kazi unayopenda kufanya zaidi iwe ya kwanza
kutendeka asubuhi. Utajkuta unatamani kuamka mapema zaidi kuwahi kazi
hiyo na siku yako itaenda vizuri
3.Andaa mapema nguo ya kuvaa siku inayofuatia, ili kuwahi jumatatu,
andaa nguo ya kuvaa jumapili usiku. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 40
(40%) ya watu huchelewa kutoka kitandani kwa kuwa walitumia muda mwingi
kupanga watavaa nguo gani.
4. Anza kupunguza dakika 20 kila siku Taratibu; Kama ulikua unaamka saa
mbili kamili, amka saa moja na dakika arobaini, baada ya siku mbili
punguza tena dakika ishirini mpaka utakaporidhika
5. Jiwekee Lengo na uwaambie watu. Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii
kwa kutaka kuwaonyesha watu kwamba umetimiza lengo lako na utajikuta
unawahi kuamka asubuhi
6. Tengeneza “appointment” (Miadi) ya kuonana na mtu asubuhi, utajikuta unawahi kuamka kwa kuogopa kumuangusha mtu huyo.
7. Kama una mtu unaishi nae, tengeneza ratiba ya pamoja kama kufanya
mazoezi, maombi, kusoma nk! Itakusaidia kukuongeza morali ya Kuwahi
kuamka.
8 Weka saa ya kukuamsha (alarm clock) mbali na kitanda ikiwa na sauti kubwa, ni vizuri ukitumia wimbo uupendao.
9. Muombe mpenzi wako akuamshe kila asubuhi, au jenga tabia ya kumpigia mpenzi wako simu asubuhi
10.Ondoa vitu Vinavyokufanya uchelewe Kuamka mfano; pombe, kahawa na kuwahi kulala usiku.
