WAZIRI wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amewaagiza
wamiliki wa viwanda vya chai nchini kununua chai ya Wakulima
wadogo kwa kuzingatia bei elekezi ya serikali na sio bei
wanayojipangia wao ya kuwanyonya Wakulima wadogo wa zao hilo la
chai nchini
Kuwa
serikali imedhamilia kuwakomboa Wakulima wadogo wa zao la chai
hapa nchini kama njia ya kukuza soko la bidhaa zitokanazo na chai hapa
nchini ya duniani ,hivyo njia pekee ni kuona Wakulima wadogo
wanaendelea kuhamasika kuongeza kasi ya kilimo hicho cha chai
ili kuviwezesha viwanda vya chai nchini kuzalisha chai kwa wingi
na ubora zaidi.
Alisema
kuwa zao la chai ni moja kati ya mazao yanayopelewa kipaumbele kama
mazao ya biashara hapa nchini na kuwa zao la chai pekee
huliingizia Taifa wastani wa dola za kimarekani milioni 50 na
kutoa ajira kwa watu milioni 2 kwa mwaka hivyo ni zao lina lina fursa
kubwa ya kuongeza wigo wa kiuchumi nchini pamoja na kuendeleza kilimo
cha zao hilo.
Waziri
Dkt Tizeba aliyewakilishwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
katika ufunguzi huo wa mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini
uliofanyika katika ukumbi wa taasisi ya utafiti wa chai (TRIT) Gwazi
Mufindi leo alisema kuwa uzalishaji wa chai nchini kwa upande wa majani
makavu ni wastani wa tani 35 kwa mwaka wakati kwa wakulima wadogo
wanazalisha wanazalisha kilo 1000 kwa hekta kwa mwaka na Wakulima
wakubwa ni wastani wa kilo 2000 za majani makavu kwa hekta kwa mwaka
ukilinganisha takwimu za nchi ya Kenya ambayo tija ni kwa mkulima
mdogo ni wastani wa kilo 2500 kwa hekta takwimu ambazo zinaonyesha
sekta ndogo ya chai nchini ipo nyuma ukilinganisha na Kenya.
“Ukuaji
wa sekta ndogo ya chai Tanzania ni mdogo sana ukilinganisha na
nchi kama Rwanda na Uganda ila kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza
uzalishaji wa tija ya chai ya Tanzania kwa kuwa nia ya kuendeleza
zao la chain a ardhi ipo ….naomba kutoa rai kwenu wadau kuweka
mipango ya kuendeleza kilimo hiki na serikali ipo nyuma yenu “
Alisema
kuwa serikali imedhamilia kushirikiana na wadau wa chai kwa kuongeza
ardhi kwa maeneo yanayolima chai hadi kufikia hekta 27000 kuwa mwaka
2021/2022 hekta kutoka 22721 kwa sasa pia kuongeza uzalishwaji wa
chai kavu kutoka wastani wa tani 32 kwa mwaka hadi kufikia zaidi ya
tani 50,000 mwaka 2021/2022 na kuongeza uzalishaji wa tija kutoka
kilo 1000 kwa mwaka hadi zaidi ya kilo 2000 za majani makavu.
Awali
mwenyekiti wa mkutano huo spika wa bunge la jamhuri ya muungano ya
Tanzania (mstaafu) Anne Makinda ambae ni mwenyekiti wa boi ya chai
nchini alisema kuwa kero kubwa ya Wakulima wadogo wa chai ni mbolea
kwa ajili ya kukuzia zao hilo kwani zao hilo Wakulima hawana ruzuku
ya serikali Kuwa mbolea inayotumika kwa zao la chai ni tofauti na ile ya mazao ya mahindi japo changamoto hiyo wanaendelea kuijadilia pamoja na serikali huku akidai kuwa chai ya Tanzania inauzwa kwa bei ndogo sana kutokana na ubora wake kuwa duni ukilinganishwa na chai ya Wakulima wadogo wa Rwanda ambao walikuwa katika vita leo wamefikia chai kavu zaidi ta tani 20,000 lakini Tanzania ambayo ilipata uhuru miaka 50 iliyopita chai haina ubora
“
Yawezekana wenzetu kwa kuwa ni Wakulima wapya wanatumia vikonyo
vipya na maeneo mapya ndio maana wanatuzidi ila sisi bado tunatumia
vikonyo vya zamani na ardhi iliyochoka “
Makinda
alisema migogoro midogo midogo inayoanzishwa na viongozi katika
maeneo ya Wakulima wa chai ni changamoto ya kurudisha nyuma kasi ya
uzalishaji wa zao la chai nchini hivyo zinahitajika jitihada za
kuondoa migogoro hiyo ili kukuza zao la chai nchini