NIMESHASEMA mara kadhaa katika makala zangu za nyuma lakini halitakuwa
jambo baya kama nikiligusia leo kidogo kwa msomaji mpya wa makala zangu,
kuwa mimi siyo mpenzi wa siasa na sifi kirii kufanya siasa katika maisha
yangu, japokuwa natambua siasa ndiyo inayoendesha dunia.
Robo tatu ya maisha yako unayoishi wewe unayesoma hapa yamesababishwa na
siasa, amani au machafuko ya nchi au jamii nyingi kwa asilimia kubwa
yanasababishwa na siasa.
Hiyo inamaanisha hata kama huipendi siasa lazima ‘uiishi’. Nimeanza na
utangulizi huo kwa kuwa nitakachokizungumza hapa kinaweza kutafsiriwa
kisiasa lakini uhalisia ni kuwa nazungumza ukweli ambao nimekuwa
nikiuona kwa muda sasa:
Tangu wajina wangu, Rais John Joseph Magufuli alipoingia madarakani na
kutangaza baraza lake la mawaziri niliona wazi mlengo wake ni kupenda
wasomi au watu waliofi ka levo fl ani ya juu kielimu.
Katika chaguzi zake za mawaziri, Rais Magufuli alifanya chaguo sahihi
katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwa kigezo cha
usomi kwa waziri husika hakikuwa kipaumbele kikubwa kama zilivyo idara
nyingine, huo ulikuwa uamuzi sahihi kwa kuwa wizara hiyo ni ukweli kuwa
inahitaji kuongozwa na mtu ambaye anaweza kuzungumza lugha na wahusika
wake wakaelewa na siyo lazima awe msomi.
Siyo kwamba wasomi hawatakiwi lakini utendaji wa waziri wa wizara hiyo,
Nape Moses Nnauye ambao amekuwa akiufanya umenivutia na ninaamini kuna
mamilioni ya watu ambao wanamuelewa anachokifanya. Achana na madongo
yake ya kisiasa ya hapa na pale ambayo ni kawaida kwa mwanasiasa lakini
haya machache niliyoyaeleza chini yanaweza kukufanya uamini kuwa Waziri
Nape anastahili kupata cheo cha kuwa waziri mkuu wa wizara yake kama
cheo hicho kingekuwepo.
Nasema hivyo kwa kuwa tukumbuke majukumu ya cheo chake yalipatikana
baada ya Rais Magufuli kuunganisha wizara kadhaa alipoingia madarakani,
hivyo mzigo alionao ni mkubwa lakini ameonyesha kuumudu:
ANAISHI MAISHA YA WASANII
Amedhuria mara nyingi matukio ya wasanii, pamoja na hivyo ametoa ushauri
mzuri, amekuwa akiwapa moyo wa kupambana, anawaonyesha njia ya kupita
na kupata mafanikio.
Amewavumilia mara kadhaa walioonyesha utovu wa nidhamu kwa kuwa wasanii
ni wasumbufu, mfano hai ni siku alipotakiwa kumkabidhi bendera Diamond,
msanii huyo alichelewa sehemu ya tukio, Waziri Nape alifi ka mapema na
kumsubiri kitu ambacho ni dharau kwa kiongozi mkubwa kama yeye lakini
alivumilia.
Amefanya ziara mitaani kusaidia masoko ya kazi za wasanii lakini ni wasanii wachache wameonyesha kumuunga mkono.
ANAJUA KUISHI NA VIJANA
Mara kadhaa amejichanganya na vijana mtaani akionyesha sapoti ya mambo
kadhaa ya kimichezo na kiburudani na wakati mwingine jukwaani, kitu
ambacho ni nadra kufanywa na mawaziri wengine ‘wasomi’.
ANASAPOTI MICHEZO
Najua Rais Magufuli siyo mpenzi sana wa michezo lakini ukweli ni kuwa
Nape amekuwa ‘link’ muhimu kati ya serikali na michezo. Amesaidia kutoa
hamasa katika timu za taifa hasa soka la vijana ambalo ndiyo msingi wa
mafanikio.
Kwenye riadha na michezo mingine napo yupo hata kama siyo mjuzi lakini
mara kadhaa nimeona akishiriki na kutoa ushauri wa kile anachoona kipo
sahihi. Matukio ya kutembelea Uwanja wa Nyamagana na Taifa katika sakata
la viti ni mfano wa jinsi alivyo ‘active’.
ANATHAMINI WANAHABARI
Hivi karibuni kulitolewa tamko la kufungwa kwa TV za mtandaoni lakini
Nape akapinga hilo kwa kusema huwezi kufungia wakati hakuna sheria, huo
ni mfumo hai na aina ya kiongozi anayetambua kile anachokiongoza pamoja
na hofu kubwa iliyopo kwa wanahabari katika serikali iliyopo
madarakani, Nape amekuwa mstari wa mbele kusimamia haki za wanahabari na
kuwatetea anapoona wana haki na mara kadhaa ameshiriki katika misiba ya
wanahabari.
Anapoona kuna wanahabari wanafanya jambo zuri imekuwa kawaida yake
kuwapongeza na siyo kusubiri wakosee tu ndiyo azungumze nao. Pia
amewatetea wasanii hadharani alipoona wanatendewa ndivyo sivyo.
ANGALIZO KWA NAPE
Pamoja na mazuri yote hayo lakini moja ya udhaifu ambao nauona kwake ni
kuwa mara kadhaa amekuwa akitoa ushauri wa mambo kadhaa, namsii sehemu
nyingine asitoe ushauri bali atoe maagizo kwa ufupi aongeza kaukali
kiduchu na asiruhusu urafi ki ukamuharibia kazi nzuri anayoionyesha.
Tags
SIASA
