Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga imengukia tena kwenye Kombe la
Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa
baada ya sare ya 0-0 na Zanaco FC kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa
uliopo mjini Lusaka Zambia.
Matokeo hayo yanamaanisha Yanga inatolewa kwa bao la ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa Mpaka mwamuzi toka Kenya anapuliza kipyenga cha mwisho timu hizo zinametoshana nguvu na kwa matokeo hayo Zanaco FC wametinga hatua ya Makundi na wanajangwani hao itabidi wasubiri droo ya kombe la Shirikisho ili kujua wanakutana na nani na kuweza kutafuta nafsi ya kuingia hatua ya makundi ikumbukwe mwaka jana walitolewa na Al-Ahly Ligi ya Mabingwa na kudondokea Shirikisho ambapo walitenga hatua ya Makundi
Tags
MICHEZO KIMATAIFA