Vyakula jamii ya nafaka ni miongoni mwa vyakula ambavyo vimejaa nishati
nyingi ikiwa ni pamoja na nyuzinyuzi na sukari. Hivyo unaweza kuweka
kwenye orodha ya vyakula anavyopaswa kula mwanaume.
Nafaka husaidia kuzalisha homoni ya testosterone kwenye damu hivyo
kumuwezesha mtu kuwa na nguvu na hivyo kuepuka tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume.
Ulaji wa vyakula vya nafaka visivyokobolewa ni muhimu zaidi kwani
husaidia kutokupa mwili wa mafuta mengi kwani mafuta mengi ndani ya
mwili huweza kuchangia kuharibu mishipa ya damu ikiwamo mishipa ya uume.
Moja ya viungo muhimu kwa wanaume ni pamoja na tangawizi ambayo husaidia
kusisimua mfumo wa mzunguko wa damu mwilini ieleweke kwamba mzunguko wa
damu unapokuwa vizuri ndani ya mwili husaidia hata damu kwenda vizuri
sehemu za viungo vya uzazi pia (uume).
Aidha, ulaji wa karanga ni muhimu pia kwani ndani ya karanga kuna madini
ya magnesium,zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za
kiume pamoja na kuamsha hisia za tendo la ndoa.
Pia matumizi ya tunda la komamanga huweza kumsaidia mwanaume kujenga
afya ya kimahusiano kutokana na tunda hilo kusaidia kuamsha mishipa ya
fahamu na hivyo kumuongezea mtu uwezo wa kushiriki tendo hilo.
