Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amezungumza na wapiga kura
wake leo katika kijiji cha Chihuta huku akieleza kuwa yeye ndiye
aliyemtafutia kura Rais John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa
mwaka 2015.
Kadhalika Nape alizungumzia tukio la kutolewa bastola alipotaka
kuzungumza na waandishi wa habari hivi karibuni na kuvitaka vyombo vya
ulinzi na usalama vichukue hatua.
“Shida niliyonayo wapiga kura wangu huyu jambazi aliyetoa silaha vyombo vya ulinzi nausalama vinafanya nini,” alisema
Alisema kutokana na tukio lile, alihitaji busara zaidi na kutulia kwani kifua chake kina mambo mengi.
Tags
Nape Nnauye
