Sakata la Richmond limechukua sura mpya Bungeni mara baada ya Mbunge wa
Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea
(Chadema) kumtuhumu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt.
Harrison Mwakyembe kuwa hakutenda haki wakati alipokuwa akishughulikia
suala hilo.
Wabunge hao kwa pamoja wamemtuhumu Waziri huyo kwa kusema kuwa wakati
akiongoza Kamati Teule ya Bunge kuchunguza Kamapuni tata ya ufuaji umeme
kuwa haikumtendea haki aliyekuwa Waziri Mkuu wa kipindi hicho, Edward
Lowassa kwakuwa hakumpatia muda wa kumhoji kitu ambacho kilipelekea
kujiuzuru.
Aidha, akijibu hoja hizo Waziri Mwakyembe amesema kuwa kama kuna mtu
yeyote ambaye ni jasiri wa kurudisha suala hilo bungeni afanye hivyo ili
aweze kulishughulikia kikamilifu na kuamaliza utata.
“Naomba nimalizie kwamba, mimi naahidi kwamba siku ambayo kuna mmoja
atakuwa jasiri wa kuleta suala la Richmond hapa, nitamuomba Rais
anipumzishe Uwaziri ili niweze kuishughulikia kesi hiyo
kikamilifu,”amesema Mwakyembe.
Hata hivyo, ameongeza kuwa Wapinzani watakuwa na kazi kubwa sana kuweza
kumsafisha mtu ambaye alikuwa ni mtuhumiwa kwa kuwa wengi hawajui undani
wa suala hilo.
Tags
Bungeni
