Mkurugenzi wa Ikolo Investment
Ltd Magidd Mjengwa akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili
kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti
wa Jukwaa la Diaspora Tanzania Mwinyimkuu Khatibu.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora
Tanzania Mwinyimkuu Khatibu akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora
kujadili kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania.Kushoto ni
Mkurugenzi wa Ikolo Investment Ltd Magidd Mjengwa
Msanii marufu wa Kundi la Orijino
Komedi Emmanuel Mgaya (maarufu Masanja Mkandamizaji) akielezea jambo
wakati wa Kongamano la Diaspora akizungumza wakati wa Kongamano la
Diaspora kujadili kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa
Tanzania.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Magidd
Mjengwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora Tanzania, Mwinyimkuu Khatibu
(kushoto). Kongamano hilo la siku mbili pia linatumika kuadhimisha
miaka 10 ya Mjengwa Blog iliyoanzishwa mnamo tarehe 19, Septemba, 2006.
Mtanzania anayeishi nchini Denmark
Bi. Edith Chenga akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Diaspora
kujadili kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo Jijini
Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili linafanyika katika Ukumbu wa
Makumbusho ya Taifa linatarajiwa kumalizika kesho tarehe 12 Aprili
2017.
Msanii marufu wa Kundi la Orijino
Komedi Emmanuel Mgaya (maarufu Masanja Mkandamizaji) akiwa na baadhi ya
washiriki wa Kongamano la Diaspora lililofanyika leo Jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kujadili nafasi ya Diaspora katika kukuza uchumi wa
Tanzania.
Mjasiriamali wa bidhaa za Dagaa
Fresh wa kutoka Ziwa Victoria ambaye pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Winlab
Bi. Winfrida Simo Tlatlaa akielezea baadhi ya washiriki wa Kongamano la
Diaspora kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo Jijini
Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akijisajili kwa ajili ya
kushiriki Kongamano la Diaspora kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi
wa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wawasilisha mada
wakiendelea na majadiliano wakati wa Kongamano la Diaspora kuhusu nafasi
ya Diaspora katika kukuza uchumi wa Tanzania katika Kongamano
lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
Tags
DIASPORA