Wasichana waliokuwa wakishika mimba kabla ya kuolewa walikua
wakisadikika kuleta aibu katika familia kwenye baadhi ya maeneo nchini
Uganda.
Kutokana na hali hiyo ya kuiletea familia fedheha, wasichana walikuwa
wakichukuliwa na kupelekwa katika kisiwa kidogo nchini humo na kuachwa
hadi kufa.
Katika jamii ya Bakiga, mwanamke anapaswa kushika mimba baada ya
kuolewa.Kuoa msichana aliye bikra kulimaanisha kupokea mahari iliolipwa
kwa kutumia ng’ombe. Mwanamke ambaye alishika mimba alionekana kutia
aibu na kuipokonya mali familia.
Bi Mauda Kyitaragabirwe mwenye umri wa miaka 80, ni mmoja ya wanawake aliyewahi kuwekwa katika kisiwa hicho cha adhabu.
”Wazazi walipogundua kwamba mimi ni mjamzito waliniweka katika mashua na
kunipeleka katika kisiwa cha Akampene. Wakati huo nilikuwa na umri wa
miaka 12 nikiishi katika kisiwa hicho kwa siku nne bila chakula wala
maji kwa siku nne”, anasimulia Bi Kyitaragabirwe.
”Nakumbuka katika Siku ya tano mvuvi mmoja alikuja na kusema atanichukua
na kunipeleka nyumbani. Nilihofu sana, na nilimuuliza iwapo alikuwa
ananidanganya na kwamba alitaka kunitupa kwenye maji, lakini alisema
hapana nakuchukua ili kukufanya mke wangu” alieza Bibi huyo kwa
mtangazaji wa BBC Swahili.
Kutokana na umbali wa eneo hilo tabia hiyo iliendelea hata baada ya
wamishenari na wakoloni kuwasili nchini Uganda katika karne ya 19 na
kuisitisha.Watu wengi wakati huo hususani wasichana walikufa kwa
kutokujua kuogelea ilikujiokoa.
Tags
Uganda
