Nimekuwa nikipata malalamiko mengi kwa akina mama wanaojifungua kwamba
matiti yao yanatoa maziwa kidogo au hayatoi kabisa. hii imewafanya
kushindwa kunyonyesha au kuingia gharama kubwa kuwanunulia maziwa ya
lactogen fomula dukani au kutumia maziwa ya ngombe.
lakini pia tukumbuke kwamba maziwa ya mama hua hayana mbadala kabisa
yaani virutubisho vinavyopatikana kwenye maziwa yale havipatikani popote
hivyo kama una shida ya kutoa maziwa basi tumia maziwa mbadala huku
ukitafuta suluhisho la maziwa yako.vifuatavyo ni vyanzo vya vya
kushindwa kutoa maziwa.
1. Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango; wanawake wengi hutumia
njia hizi baada ya kujifungua bila shida yeyote lakini kuna baadhi yao
njia hizi huingilia mfumo wao wa kutoa maziwa hasa zikitumika kabla
mtoto hajafikisha miezi sita. hii husababishwa na kuongezeka kwa homoni
za uzazi yaani progesterone na oestrogen ambazo hushusha homoni ya kutoa
maziwa yaani prolactin hormone.kama umekumbwa na hali hii basi acha
mara moja njia hiyo na utumie njia zingine kama kondom,kalenda au njia
nyingine isiyotumia dawa.
2. Matatizo ya kimaumbile; baadhi ya wanawake matiti yao
hayakukamilika wakati wamakua yaani yanakua na upungufu wa vitu muhimu
vinavyohifadhi maziwa kwenye matiti kitaalamu kama grandular tissues hii
hufanya maziwa yatoke kwa shida sana.mama anashauriwa akamue maziwa
wakati wa kunyonyesha na mara nyingi mtoto wa pili mpaka watatu
wakizaliwa matiti haya yanakua yameshazoea hivyo hayasumbui tena kutoa
maziwa.
3. Upasuaji wa matiti; kama mama ameshawahi kupasuliwa matiti
yake kwa shida yeyote labda majipu, ajari, upasuaji wa kuongeza au
kupunguza matiti basi kwa namna moja au nyingine hii inaweza kuharibu
mfumo wake wa matiti kupitisha maziwa na kujikuta hatoi maziwa ya
kutosha.ukiwa na shida hii utahitaji kutumia maziwa mbadala kwa mtoto.
4. Matumizi ya dawa; wakati wa kunyonyesha mama anaweza kuugua na
kutumia dawa fulani fulani ili apone ugonjwa alionao lakini kuna
baadhi ya dawa ni hatari kwani hushusha kiwango cha maziwa. mfano dawa
za kama bromocriptine,methergine,pseudoephredine.
5. Matatizo ya homoni za uzazi; matatizo ya homoni kua juu sana
au kua chini sana yanaweza kusababishwa na magonjwa ya ovari, kisukari
na kadhalika. pia magonjwa yeyote ya homoni yanayochelewesha mtu kupata
mimba huweza kuzuia maziwa pia. ni vizuri ukaonana na daktari kupima
kiwango cha homoni na kupata matibabu.
6. Kutonyonyesha usiku; wakati wa usiku homoni inayohusika na
kutengeneza maziwa yaani prolactin hutengenezwa kwa kiwango cha juu sana
lakini pia ili mtoto alale usiku mzima bila kusumbua lazima anyonye
vizuri usiku.kutonyonyesha usiku hupunguza homoni hii na kumfanya mama
atoe maziwa kidogo sana siku inayofuata.
7. Kutonyonyesha vya kutosha; kawaida mama anatakiwa anyonyeshe
angalau mara kumi ndani ya masaa 24, sasa mwili hutengeneza maziwa
unapohisi matiti hayana kitu na kama mwili ukihisi matiti yana maziwa
muda mwingi basi unajua maziwa hayahitajiki sana na kuanza kupunguza
kiasi cha kutoa maziwa.
8. Kutokula vizuri; maziwa anayotoa mama yanatengenezwa na
chakula anachokula wala sio miujiza fulani hivyo kipindi hiki mama
anatakiwa ale mlo kamili yaani matunda, protini ya kutosha, wanga, mboga
za majan na maji mengi i na ikiwezekana atumie virutubisho
vinavyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kuongeza maziwa.
9. Matumizi ya vyakula mbadala; miezi sita baada ya kuzaliwa
mtoto anatakiwa anyonye tu bila kupewa kitu chochote, kuna watu hua
wanawapa maji wakidai eti watoto walisikia kiu sio kweli.sasa kuanza
kumchanganyia maziwa ya ngombe na yale ya dukani kutamfanya anyonye
kidogo kwako na mwili utapunguza kiasi cha maziwa yako...hivyo siku
ukikosa mbadala utajikuta huna maziwa kabisa.
10. Mtoto kushindwa kunyonya; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba
maziwa yakitoka mengi na mwili unatengeneza mengi zaidi na kama mtoto
hanyonyi vizuri basi na maziwa hutoka kidogo zaidi.hali hii inaweza
kusababishwa na dawa ya usingizi ambayo alipewa mama wakati wa
kupasuliwa ambayo huamuathiri mtoto pia, au matatizo ya kuzaliwa nayo
kama tongue tie[ulimi kushikwa chini ya mdomo, hii inaweza kurekebishwa
na daktari] au mtoto kuugua.
Tags
AFYA
