Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amesema jeshi hilo linawasaka
watu wanaofurahia mitandaoni na kukebehi baada ya askari wake kuuawa.
IGP ameyasema hayo wakati Miili ya Askari nane wa Jeshi la Polisi ikiagwa leo Mkoani Pwani.
IGP Mangu amesema, tulitumue tukio hili kama changamoto, ili tupeane
nguvu badala ya kukatishana tamaa. Kuna watu wameanza kukejeli kwenye
mitandao baada ya hili tukio kutokea, mheshimiwa Waziri nakuhakikishia
tutawasaka hao wanaoendeleza kejeli badala ya kutupa pole wanakejeli na
wengine wanafurahia.
Na mtu wa namna hii anefurahia si mwingine isipokuwa ni mhalifu kama
huyu aliyefanya tukio hili baya, nao tutawashughulikia kwa mujibu wa
sheria tutakapowapata.
Ila tu niombe wananchi tutumie tukio hili kama changamoto na tutiane
nguvu ili mwisho wa siku tuweze kushinda hii vita ya uhalifu kwa sababu
hakuna mtu anayependa uhalifu na wote tunapenda amani.
Tags
IGP
