Hamis kigwangalla leo ameamua kufunguka kwa mwanaharakati Mange Kimambi
huko Instagram baada ya mwanadada huyo kupost picha na maombi kibao
kutoka kwa wananchi wakimwomba awasaidie kufikisha vilio vyao
serikalini.
Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya mwanadada Mange kufululiza
kupost picha na post mbali mbali zikionyesha hali mbaya ya huduma za
afya kwenye baadhi ya hospitali zetu.
Nyingi ya post zinaonyesha jinsi wanawake kwenye baadhi ya hospitali
kubwa ( including MUHIMBILI ) wakiwa wamelala chini sakafuni na watoto
wao baada ya kutoka kujifungua, na baadhi ya post nyingine ni message
anazotumiwa na watu mbalimbali wakilalamika jinsi wanavyopata tabu
kupata huduma za afya mahospitalini .

