Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha
kulinda ikolojia ya mto Ruaha Mkuu ambaye pia Mkurugenzi Idara ya
Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiongea na
Watendaji wa Wilaya ya Mufindi (haapo pichani) katika Mkoa wa Iringa
wakati wa mkutano kati ya Wajumbe wa Kikosi Kazi na Watendaji wa Wilaya
hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa Wialaya ya Mufindi wakisikiliza maoni
mbalimbalimbali ya Wajumbe wa kikosi kazi cha kuimarisha ikolojia ya Mto
Ruaha Mkuu kilchoteuliwa na Mkamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa
Tanzania (hawapo pichani) .
Katibu Tawala wa Mkoa wa mbeya
Bibi Mariam Mtunguja akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikosi
kazi hiko kilipotembelea Wilaya ya Mufindi.
………………
Halimashauri ya Wilaya ya Mufindi
imepewa mwezi mmoja kuhakikisha vyanzo vote vya maji vinaainishwa,
kutambuliwa na kuhakikisha shughuli zote zinazosababisha kukauka kwa
vyanzo hivi zinaachwa mara moja. Aidha Halmashauri imeangizwa
kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi
ili kutenga maeneo ya mashamba ya kulima chakula na maeneo ya kupanda
miti ili wananchi wawe na ardhi ya kujitosheleza na endelevu ya kilimo
cha mazao ya chakula. Kwa sasa miti inapandwa kila sehemu na vijiji
vingi sasa havina maeneo ya mashamba ya kilimo cha vyakula ya kutosha
na hivyo kusababisha wananchi kuendelea kuvamia mabonde kwa ajili ya
kilimo cha Vinyungu.
Maagizo haya yametolewa na
Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Taifa cha kunusuru na kuweka
mikakakti endelevu ya kulinda ikolojia ya mto Ruaha Mkuu, ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana
Richard Muyungi alipokua akiongea wakati wa mkutano wa Kikosi kazi
pamoja na uongozi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Aidha ameangiza
mpango kazi wa utoaji wa elimu kwa wananchi katika hali endelevu kwa
vijiji vyote 121 ambao utawaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza
mazingira ya Mto Ruaha mkuu na vyanzo vote vya maji uwasillishwe
katika sekretariat ya kikosi kazi ndani ya siku nne ili kujua ni jinsi
gani wilaya itahahakikisha suala la elimu kwa umma linakuwa endelevu.
Wakichangia katika kikao
hiko, Wajumbe mbalimbali wa kikosi kazi hiko wamesisitiza juu ya
Watendaji wa Wilaya hiyo kuwa makini katika utendaji wao wa kazi na
kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria za ardhi na Mazingira ili
kuwezesha ikolojia ya mto Ruaha mkuu inatunzwa vizuri. Katibu Tawala wa
Mkoa wa Mbeya Bibi Mariama Mtunguja, alisisistiza haja ya kila mtendaji
kujituma na kuacha kutoa visingizio vya ukosefu wa fedha kwa kila kazi
ambazo hazijafanyika hata zile ambazo ni wazi hazihitaji fedha yoyote.
Alihoji kwa nini hata kazi ya kuweka mipaka ya vyanzo via maji
vinavyojulikana kwa kupanda miti ya asili katika mipaka hiyo
kunasubiri fedha ya serikali kuu.
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya
ya Mufindi Mhe. Jamhuri William alishukuru kikosi kazi hiko kwa kufika
katika Wilaya yake na ameahidi kusimamia na kuyafanyia kazi maagizo
yote yaliyotolewa na kikosi kazi hiki. Aidha Viongozi mbali mbali
wakiwemo Madiwani na Wevyeviti wa Halmashauri wamekubaliana na maelelezo
ya kikosi kazi kuhusu hatua kali kwa watakaokaidi maagizo ya serikali
kuhusu kunusuru mto Ruaha mkuu ili kunusuru mazingira na kuwepo kwa
uhakika wa maji kwa watumiaji wote.
Kikosi kazi hicho kimeundwa na
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni
jitahada za kuweza kuokoa ikolojia ya mto Ruaha mkuu ambao unazidi
kuharibika siku hadi siku kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji
kutokana na shughuli mbali mbali za ki binadamu katika vyanzo vya maji
ya mto huu.
Tags
MTO RUAHA MKUU