Amezungumza kuhusu Diamond kumshambulia katika wimbo wake, na amesema
mtu wa Mungu huwa hashambuliwi na binadamu. Amedai kuwa atazungumzia
kuhusu Diamond kujiunga Chama cha Freemason na alijiunga lini, wapi na
kafara gani alitoa ili aweze kukubaliwa kujiunga. Mchungaji Gwajima
alishusha pumzi na kusema hatamoiga Diamond baada ya Diamond kujirudi na
kumuomba msamaha Askofu Gwajima. Mchungaji Gwajima ameinukuu Biblia na
kusema inakataza kumchapa/kumpiga mtu aliyeomba msamaha.
Kuhusu Makonda, Askofu Gwajima amesema Bashite anahusika kwa utekaji wa
Msanii Roma, amesema mtu huyo huyo aliyevamia kituo cha Habari Clouds
Media ndiye huyo huyo mtekaji kwasababu ana mtu wa kumkingia kifua. Pia
amemtaka Bashite akajifiche huko kwenye Balozi kama Congo na kwingineko
ili akajiendeleze na Elimu ya QT au MEMKWA maana akibako hapa Tanzania
watu watamgawana akiingia mtaani.
Askofu Gwajima kuhusu Halima Mdee kumtukana Spika wa Bunge la Jamhuri,
amemtaka Mbunge Halima Mdee kuacha mara moja kumtukana Spika maana ni
moja ya Mhimili wa Dola. Amesema kuwa Halima Mdee asipoomba msamaha basi
Jumapili ijayo atamchapa ipasavyo.
Tags
Askofu Gwajima
