Timu ya KRC Genk anayocheza
Mtanzania Mbwana Ally Samatta imeshindwa kutamba ugenini dhidi ya
wenyeji CeltA Vigo baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-2 mchezo wa
robo fainali wa Europa League.
Kwa matokeo hayo Genk wamejiweka
katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwani wanahitaji ushindi wa goli
moja tu ili waweze kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.
Magoli ya KRC Genk yalifungwa na
Jean Boetius dakika ya 10 na Thomas Buffel aliyeingia akitokea benchi
dakika ya 68, kwa upande wa wenyeji magoli yao yalifungwa na Pione Sisto
dakika ya 15, Iago Aspas dakika ya 17 na John Guidetti dakika ya 38,
kipigo hicho kinailazimu Genk katika mchezo wa marudiano Luminus Arena
April 20 itabidi wapate ushindi wa kuanzia goli 1-0 ili wafuzu
nusu fainali.
Matokeo Mengine ya Europa League:
Tags
MICHEZO KIMATAIFA