tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 9 mpaka 15 ya binadamu duniani
wanasumbuliwa na matatizo ya kukosa usingizi, tatizo hili ni moja ya
matatizo mabaya sana ambayo huweza kumfanya mtu ashindwe kutambua
anaishi ulimwengu wa aina gani kwani muda mwingi anakua ni mchovu na
hawezi kufanya kitu chochote kwa umakini.
ugonjwa wa kukosa usingizi huwasumbua zaidi watu wazima kwanzia miaka 40
kwenda mbele hasa wanawake kuliko wanaume japokua unaweza pia
kuwashambulia vijana wadogo kulingana na matatizo mbalimbali lakini watu
wazima sana ndio waathirika wakuu wa shida hii.
kuna aina tatu za matatizo ya kukosa usingizi
kukosa usingizi kunaweza kuja kwa aina tatu yaani kukosa usingizi
ghafla, kukosa usingizi mara moja moja au kukosa usingizi kwa muda mrefu
sana.
hali hii ya kukosa usingizi husababisha matatizo mbalimbali kama
kunenepa,kupoteza kumbukumbu, kushindwa kufaulu darasani, kushindwa kua
makini na kazi, kuchoka sana,wasiwasi, mgandamizo wa mawazo, na hatari
ya kupata magonjwa yasiyotibika kama ugonjwa wa presha na kisukari.
nini husababisha kukosa usingizi?
watu sababu mbalimbali huweza kukosa usingizi kama ifuatavyo
mabadiliko ya mfumo wa maisha; hii inaweza kusababishwa na kazi
unayofanya kama kuanza kufanya kazi usiku...kazi za ulinzi, kazi za
uuguzi, na kadhalika lakini pia kuishi sehemu yenye kelele sana,kusoma
sana usiku, baridi sana au joto sana.
matatizo ya kisaikolojia; watu wenye msongo wa mawazo
unaosababishwa na matatizo mbalimbali kama kukosa ajira, matatizo ya
kiuchumi, kuvunjika kwa mahusiano, magonjwa ya akili, kua na wasiwasi
sana wa mambo yanayokuja, wasiwasi wa kuibiwa mali zako ukiwa ndani
umelala hasa wamiliki wa magari na mali zinazolala nje.
magonjwa mbalimbali; kuugua magonjwa fulani fulani huweza
kumfanya muhusika kukosa usingizi kabisa wakati wa kulala mfano pumu au
asthma, magonjwa ya moyo, maumivu makali ya sehumu ya mwili,kiharusi,
madonda ya tumbo, maumivu ya jino, na kansa mbalimbali.
mabadiliko ya kiwango cha homoni; hii hutokea wakati wa kipindi
cha hedhi ambapo kunakua na mabadiliko madogo ya homoni za uzazi,
kipindi cha ujauzito na ugonjwa wowote unaobadilisha kiwango hicho.
teknolojia; kulala na simu na kuendelea kuchati, tv au komputa
chumba cha kulala,michezo ya gemu na kadhalika..hii imeathiri sana watu
wengi kwani siku hizi kabla ya kulala utamkuta kila mtu anachezea simu
angalau saa moja.
dawa mbalimbali; kuna dawa nyingi sana ambazo zimetajwa kunyima watu usingizi kama ifuatavyo
dawa za presha mfano propanolol,metoprol,losartan,atenolol,metoprol, captopril,enapril na solatol,lisinopril
dawa za msongo wa mawazo mfano fluoxetine na paroxetine
dawa za kushusha kiwango cha lehemu mwilini mfano simvastatin,rosuvastatin,lovastatin.
dawa za kupunguza maumivu ya mifupa mfano chrondotin na glucosamine
dawa za kutibu aleji mfano cetrizine
sababu zingine mfano kulala sehemu yenye kelele nyingi, kulala na mtu
anayekoroma usiku, kulala sehemu yenye wadudu kama mbu na chawa
watu gani hasa wanasumbuliwa na shida hii?
- watu wanaosafiri sana
- watu wanaofanya kazi za usiku
- wazee sana
- wanaotumia dawa mbalimbali
- vijana wadogo ambao mahusiano na ajira ni tatizo kubwa kwao.
- wanawake waliofika mwisho kuona siku zao za hatari
- watu wenye magonjwa ya akili
dalili za kukosa usingizi ni kama ifuatavyo..
- kushindwa kulala kabisa
- kuamka usiku sana na kukosa usingizi
- kuamka mapema sana kuliko kawaida
- kusikia usingizi baada ya kuamka asubuhi
- kuchoka sana mchana wakati wa kazi
- mgandamizo wa mawazo na kua na wasiwasi sana
- kukosa umakini wakati wa kazi
- kupata ajari za wakati wa kutumia vyombo vya usafiri.
- kuumwa kichwa sana
- kuharisha, kichefuchefu na kukosa hamu ya chakula
- kushindwa kuongeza na watu
vipimo vinavyofanyika
daktari humuuliza mgonjwa mbalimbali kuhusu tatizo lake la kukosa
usingizi, vipimo mbalimbali pia huweza kuchukuliwa pia kutafuta magonjwa
ambayo yanaweza kumkosesha mtu usingizi.
kwa mtu kugunduliwa na tatizo hili lazima awe amemaliza mwezi mmoja bila kupata usingizi unaoeleweka
vipimo vya kisasa zaidi kama polysmonography huweza kutumika kwa mgonjwa aliyelazwa kupima usingizi wake wakati wa usiku
matibabu;
mara nyingi matatizo ya kukosa usingizi hua yanaaisha pale chanzo cha
tatizo kinapotibiwa kwa mgonjwa husika, hivyo mara nyingi matibabu
yanalenga kuondoa chanzo cha tatizo hili.
matibbu yamegawanyika katika matibabu yasiyohusu dawa yaani non
pharmacological treatment na matibabu yanayohusu dawa yaani
pharmacological treatment kama ifuatavyo
matibabu yasiyohusu dawa[ non pharmacological treatment]
ongeza nidhamu ya usingizi; epuka kulala sana au kidogo sana,
epuka kulala na njaa, epuka kunywa kahawa na kuvuta sigara wakati wa
kulala, hakikisha ratiba yako ya kulala haibadiliki, hakikisha unalala
kwenye mazingira rafiki ya usingizi yaani bila kelele au usumbufu
wowote.
muone mtalaamu wa ushauri; unaweza kuonana na mshauri akakusaidia kutatua tatizo lako la kisaikolojia linalokusumbua, huduma hiyo tunatoa pia.
epuka vitu mambo ya teknolojia yanayozuia usingizi; tabia ya kua na tv chumba cha kulala, laptop kitandani au kutumia simu usiku kabla ya kulala huweza kukunyima usingizi.
epuka kulala mchana; tabia ya kulala mchana huweza kukunyima kabisa usingizi wakati wa usiku, hivyo kaa mbali kabisa na kitanda wakati wa mchana.
pata matibabu ya tatizo lolote la kiafya linalokusumbua; kama
kuna ugonjwa wowote unakusumbua hakikisha unatibiwa, kama ni ugonjwa
usiotibika basi hakikisha unafuata matibabu ya kupunguza makali yake.
pata suluhisho la tatizo la kisaikolojia;kama una msongo wa
mawazo sababu ya kuachwa kwenye mahusiano huwezi kulala kabisa, kama una
matatizo ya kiuchumi, umefiwa, au msongo wowote wa mawazo basi
hakikisha unapata suluhisho lake.
matibabu ya dawa[pharmacological treatment]
wakati mwingine chanzo cha kukosa usingizi kinaweza kua nje ya uwezo wa
muhusika yaani hawezi kutatua tatizo linalomsumbua hivyo anahitaji
matibabu ya dawa ambazo angalau zitampa usingizi alale kama ifuatavyo :-
ant depressant; mfano fluoxetine na paroxetine ,anthistamine
ramelteon ,melatonin
