
Mahusiano mazuri kwa wanandoa au watu walio kwenye mahusiano ya
kimapenzi ni moja ya mambo yanayochangia wahusika pia kuwa na afya njema
na hata kuepuka baadhi ya matatizo kiafya.
Leo nmeona nikuletee mambo matano muhimu ambayo mwanamke hupenda atimiziwe na mume wake.
1. Kudekezwa & Kubembelezwa
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, lakini pia
wengi hupenda kuungwa mkono katika maamuzi yao au mawazo yao. Hivyo basi
ili mwanaume uweze kumteka mwanamke wao ni lazima ujitahidi kuwa
mkarimu na mwenye lugha nzuri za kubembeleza kwa mkeo.
2. Kusikilizwa shida
Wanawake hupenda pale wanapoeleza shida zao wasikilizwe vizuri na
kutatuliwa matatizo yao. Inawezekana hayo matatizo yakatatuliwa kwa
kuwezeshwa kifedha au hata ushari pia wakati mwingine.
3. Kuwa mstari wa mbele
Wanawake muda wote hupenda kuoneshwa kuwa wao ni wathamani kuliko
wengine hivyo huhitaji kuwekwa mstari wa mbele katika mambo yao. Hali
ambayo huwafanya wao kuhisi wanapendwa zaidi.
4. Kufurahishwa kwenye ndoa
Hakikisha wewe kama ni mwanaume basi katika sekta hii uwe umekamili
kiasi cha kutosha yaani hata kama huna fedha, lakini hakikisha eneo hili
unaliweza vizuri na unalifanya kwa ufanisi zaidi kila unapokutana na
mkeo. Kwani uwapo dhaifu eneo hili basi ni rahisi sana kuyumbisha
mahusiano yenu au ndoa yenu.
Kimsingi wewe kama mwanaume ni lazima utambue kuwa unawajibu wa kuhakikisha unamridhisha mpenzi/mke wako katika tendo hilo.
5. Nafasi ya kuzungumza
Kwa kawaida wanawake hupenda zaidi kujieleza kuhusu hisia zao au mambo
yao kwa wale wanaohisi wanawapenda, hivyo mwanaume lazima uhakikishe
unatenga muda wa kuzungumza na mpenzi wako na kumsikiliza kuhusu mambo
yake na kuyafanyia kazi pale yanapoonekana yanawezekana.
Kimsingi mambo hayo yote au machache kati ya hayo yakitokea yakakosekana
ndani ya ndoa kwa mda wa kipindi fulani huweza kupelekea mwanamke
kuondoka na ndoa kuvunjika hivyo ni muhimu kwa wanaume kuyazingatia
hayo.