Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe
amesikitishwa na vitendo walivyofanyiwa wasanii wa muziki Roma Mkatoliki
na wenzake huku akisema hawezi kukubali kuona mambo kama hayo yakiwa
yanaendelea kutokea.
Akizungumza na wanahabari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema
kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi
kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu
sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya
wizara yake
"Hiki kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi
kukubali kitu kama hiki kiendelee kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu
sana, nitajitahidi nipate majibu kabla ya bajeti yangu Bungeni". Alisema
Dk. Mwakyembe
Hata hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka wananchi waache tabia ya kuamini
kila maneno yanayosemwa na watu ambao hawana ujuzi katika masuala ya
uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda vyombo vya dola viweze kufanya
kazi zake kwa ufasaha.
"Nilishasema kuwa nimeagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili
ajulikane aliyewafanyia hivi wakina Roma kama ni nani kama wa dola
ntadili naye, tuache uchunguzi ufanyike, tuache kupiga ramli".
Alisisitiza Mwakyembe
Pia Waziri huyo mwenye dhamana na wasanii ametoa ujumbe kwa vyombo vyote
vilivyopo chini ya Wizara yake kutofanya mahojiano yoyote yanayowahusu
wasanii hao bila ya kuwepo taarifa kamili kutoka kwake.
Kwa upande mwingine Roma ambaye ambaye amesimulia tukio lilivyokuwa
amesema kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi kwa kuwa kila kitu
amekwisharipoti polisi kila kitu, na kwamba kuna mambo akiyaweka
hadharani atakuwa anaingilia upelelezi wa polisi.
Pia amesema hawezi kujua kama kweli tukio hilo lililowatokea
linahusiana na muziki kwa kuwa ameweza kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao
wa ndani ambaye hana hata chembechembe za uimbaji.
