Mwezeshaji kutoka asasi isiyo ya
kiserikali ya Feasible Resource, Yared Babona akitoa mada katika mafunzo
ya urasimishaji na mpango wa biashara kwa wakulima na wasindikaji
mkonge kutoka wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na Meatu mkoani Simiyu.
Washiriki wakifuatilia mafunzo ya
urasimishaji na mpango wa biashara kwa wakulima na wasindikaji mkonge
kutoka wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na Meatu mkoani Simiyu.
Meneja Mradi wa REDESO Wilaya ya Kishapu, Charles Buregeya akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki wakiendelea kufuatilia mafunzo hayo kutoka ka mwezeshaji.
Mwezeshaji kutoka asasi ya
Feasible Resource, Yared Babona akiendelea kutoka mada kwa washiriki wa
mafunzo hayo (hawapo pichani).
Washiriki wa mafunzo ya ya urasimishaji na mpango wa biashara wakimsikiliza mwezeshaji.
………………………..
Asasi isiyo ya kiserikali ya
Msaada na Mandeleo ya Jamii (REDESO) imetoa mafunzo ya urasimishaji na
mpango wa biashara kwa wakulima na wasindikaji mkonge kutoka wilaya ya
Kishapu mkoani Shinyanga na Meatu mkoani Simiyu.
Mafunzo hayo yaliyofanyika
wilayani hapa kwa ushirikiano pia na Shirika lisilo la kiserikali la
OXFAM yalilenga kuwajengea wakulima hao uwezo na mbinu za kuongeza
faida.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mafunzo hayo, Meneja Mradi wa REDESO Wilaya ya Kishapu, Charles Buregeya
alisema washiriki wanawezeshwa kuwa na mpango kazi na kusajili biashara
zao.
Alisema wengi wa wakulima na
wasindikaji wa zao hilo linalofanya vizuri katika wilaya hizo wanakosa
mbinu za biashara hivyo kupitia mafunzo watakuwa na uwezo wa kutafuta
masoko.
Buregeya aliongeza kuwa ili waweze
kuwa na uwezo wa kutafuta masoko mafunzo hayo yanajumuisha pia kupatiwa
mbinu za ushawishi na kuweza kuuza bidhaa zao na kupata faida.
Alisema pia mafunzo hayo
yaliyotolewa na mwezeshaji kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya Feasible
Resource, Yared Babona yanalenga kuwawezesha washiriki kulifanya zao
hilo kuwa na tija na manufaa zaidi.
Redeso inafanya kazi na mamlaka za
Serikali za Mitaa katika halmashauri hizo mbili za wilaya kwa kuendesha
mafunzo hayo kwa wilaya hizo mbili kupitia wanachama wa Shirikisho la
Wasindikaji Meatu na Kishapu (SHIWAMKI).
“Ukweli ni kuwa shirikisho hili
bado ni changa lakini kutokana na mazungumzo tuliyofanya na Bodi ya
Mkonge Tanzania (TSB) lina uwezo wa kufanya vizuri katika ukanda huu wa
Ziwa Victoria endapo hatua za haraka zikichukuliwa,” alisema.
Hivyo, alisema ili hayo yote
yaweze kufanikiwa taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa makundi ya
wakulima na wasindikaji wa zao hilo ambalo limekuwa likifanya vizri
katika ukanda huo.
Mkonge ni mojawapo ya mazao
yaliyoonesha mafanikio makubwa katika Wilaya ya Kishapu kutokana na
kuhimili hali ya ukame ambayo huwa ni changamoto kubwa kutokana na uhaba
wa mvua.
Hivyo halmashauri ya wilaya hiyo
inachukua hatua mahsusi za kuhamasisha kilimo hicho kwa kuwa kimeonesha
tija kubwa hivyo kinaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya
kilimo.
Tags
USNDIKAJI