Sakata la kufukuzwa nchini la bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni.
Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga(Chadema) akizungumza bungeni leo,
aliitaka serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi
huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliliambia bunge kuwa
serikali ina mamlaka yote katika masuala ya kidiplomasia na hivyo bunge
haliwezi kuhoji sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.
Tags
Bungeni