Sakata la pointi tatu ambazo Simba SC ilipewa na Kamati ya Saa 72
kutokana na kile kinachodaiwa Kagera Sugar ilichezesha mchezaji Mohamed
Fakhi akiwa na kadi za njano tatu kinyume na sheria za ligi kuu msimu
2016/17 limechukua sura nyingine baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania kusema bado ushahidi
haujakamilika ipasavyo hivyo.
Akitangaza mbele ya waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa amesema kikao cha jana kilikuwa
maalumu kwa ajili ya kumaliza kazi ilianzwa na Kamati ya Saa 72 na sio
kuiharibu maamuzi yake ambayo ilitoa.
“Mashahidi wengi hawajaweza kufika hivyo lazima usubiri mpaka waletwe
ili kukamilisha kazi. Pia nyaraka muhimu haziletwa. Kamati ya Saa 72
haina nguvu ya kustafiri sheria hivyo kinachofanyika sisi (Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji) tunamalizia ilipoishia,” alisema Mwesigwa.
Mwesigwa ameongeza kuwa ni lazima kuliweka suala hili vizuri kwa maslahi
ya siku za usoni hivyo wakienda nalo kwa pupa litakuwa na athari katika
siku zijazo katika soka la Tanzania.
Kikao hicho kimeahirishwa hadi leo Aprili 19 mwaka huu.
