Timu ya Simba ikifanya mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na timu ya Geita Gold Sport Mchezo ambao umechezwa kwenye shule ya msingi ya Waja.
| Timu ya Geita Gold Sport akijiweka sawa kucheza mchezo wa kirafiki na Simbo. |
| Timu zote mbili zikiingia uwanjani kukabiliana. |
| Mgeni Rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba. |
Mgeni Rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Geita Gold Sport.
Mchezo
wa kirafiki baina ya simba Sport club na Geita Gold sport ya
Mkoani Geita umemalizika kwa timu ya simba kuifunga Geita gold mabao
7-0, ambapo wekundu hao wa msimbazi wamelilipiza kisasi kutokana na
mchezo wao wa kirafiki mwaka jana ambapo simba walichezea magoli matatu
kwa moja.
Ushindi
huo umetokana na mabao ya viungo Said Hamisi Ndemla, Pastory Athanas,
Mwinyi Kazimoto moja kila mmoja wakati Mohammed Ibrahim alifunga mawili
sawa na
mshambuliaji Muivory Coast, Frederick Blagnon.
mshambuliaji Muivory Coast, Frederick Blagnon.
Simba imeweka kambi Geita ikitokea Bukoba, ambako Jumapili ilichapwa 2-1 na wenyeji Kagera
Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba.
Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba.
Na
Wekundu hao wa Msimbazi wanajiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu, dhidi
ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza wikendi hii na watamaliza
mchezo wao kanda ya ziwa na timu ya Toto Africans
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Tags
SIMBA SC