
Kuna kitu ambacho Rais amekuwa akikisema mara kwa mara na ninaamini kuna
ukweli wake. Kwamba, siyo wote wanaolalamikia utawala wake wanafanya
hivyo kwa sababu wanataka afanikiwe. Ni kweli pia kuwa wapo
wanaolalamika kwa sababu wanafikiri kuna labda namna bora ya kufanya
mambo fulani fulani. Lakini, kuna masuala ambayo anayafanya ambayo bila
ya shaka Watanzania wako nyuma yake.
"Tulionewa sana
Tumechezewa sana
Tumedharauliwa mno"
Siku ya Krismasi ya mwaka juzi gari langu dogo la Nissan Maxima
lilizimika kwenye eneo la kuegeshea magari hapo hapo kanisani. Bahati
nzuri nyumba yangu ni dakika kumi tu kutembea kutoka kanisani. Kila
namna ya kuliwasha tena haikuwezekana. Nilipowaita mafundi wakaniambia
tu kuwa injini imekufa! Hakukuwa na jinsi isipokuwa kuweka injini
nyingine!
Kuna ukweli kwamba wakati mwingine hata gari zuri kiasi gani inabidi
ulipeleke kufanyiwa matengenezo ya kawaida. Lakini, kuna wakati gari
linahitaji matengenezo makubwa. Katika kufanya matengezo makubwa gari
linaweza kukongolewa kabisa, injini kushushwa, vilivyochakaa kutolewa,
n.k Mtu yeyote atakayeliona gari likiwa kwenye matengenezo makubwa
anaweza kudhania ndio mwisho wake; kwamba limeharibiwa. Lakini
likiunganishwa tena na kuanza kazi linakuwa katika ubora zaidi kuliko wa
awali. Sasa watu wakilalamika tu kusema kuwa gari limeharibiwa wanaweza
kuwa sahihi kwa sababu wanaweka mkazo katika mwonekano likiwa kwenye
matengenezo!
Kazi kubwa kwa Magufuli ni kuwafanya watu waamini kuwa analitengeneza
gari hilo na kuwa matengenezo haya ni kwa ajili ya ubora wa baadaye. Na
kwamba katika kufanya hili hatoonea huruma kuondoa visivyo faa na hata
ikibidi kuishusha injini na kuweka injini nyingine. Katika matengenezo
ambayo anaendelea kuyafanya Tanzania ambayo sisi wengine tuliyaita
"mabadiliko ya kweli" na sasa naomba kupendekeza yaitwe pia "mabadiliko
sahihi"kuna vitu ambayo anatakiwa kuendelea navyo na kuvifanya vizuri
zaidi lakini kuna vingine ni lazima avifanye kama hivyo vingine
vinatakiwa kufanikiwa.
Kufumua Idara ya Usalama wa Taifa ni moja ya mambo muhimu sana ya kuweza
kufanikisha maeneo mengine yote. Mgonjwa wa moyo hata kama ana matatizo
mengine ya mguu na meno; au hata kama ana matatizo ya tumbo; anaweza
kuyashughulikia hayo mengine yote lakini bila kushughulikia tatizo kubwa
la moyo mengine yanaweza kushughulikiwa lakini mwisho wa siku ni moyo
utakaoamua kama hayo mengine yana nafasi ya kufanikiwa! Usalama wa Taifa
ni moyo wa taifa! Hautakiwi hata kwa siku moja uonekane unapiga kwa
matatizo, au una matatizo mengine...
Inshallah, wiki ijayo nitaendeleza hoja hii ya mabadiliko makubwa ya
Idara. Tusisubiri watu wa nje watushunikishe kufanya mabadiliko. Baba wa
Taifa alikuwa na msemo ambao wengi labda wameusahau (hii ilikuwa mara
baada ya uhuru) kuwa "Tanzania ni ya Watanzania na Watanzania ni Wote -
Tanzania is for Tanzanians and Tanzanians are All". Msemo huu ulikuwa
unasisitiza tu kuwa hakuna mwenye Utanzania zaidi ya Watanzania wengine.
Kila Mtanzania - haijalishi kabila, dini, rangi, uwezo, hadhi, mahali,
hali au umbali - ana haki sawa na Mtanzania mwingine yeyote. Hakuna
Mtanzania wa juu zaidi!
Tags
RAIS MAGUFULI