Lowassa yuko kimya kabisa wala hazungumzii mambo yalivyokuwa ndani ya
Serikali tangu atoke kwenye Uwaziri Mkuu ambao alijiuzulu mwaka 2008.
Kuna baadhi ya watu wanautafsiri ukimya wa Lowassa kama ni woga ama
kukiri kwamba alishiriki kwenye "Ufisadi" wa Richmond. Lakini Lowassa
alikuwa ni Waziri Mkuu na kwa kawaida Waziri Mkuu hula kiapo cha
uaminifu na cha kutunza siri za Baraza la Mawaziri ambacho kipo
Kisheria.
Lakini pia kwa mujibu wa Katiba yetu Ibara ya 52 ambayo inataja majukumu
na mipaka ya kazi za Waziri Mkuu. Waziri Mkuu anatakiwa kufanya kazi
kwa kufuata maelekezo ya Rais aliyeko Madarakani. Ukisoma pia Ibara ya
35 (i) wafanyakazi wote wa serikali wanafanya kazi kwa niaba ya Rais.
Jambo la Richmond kupewa Tenda ya kuleta Jenereta za Kufua Umeme
lilianzia kwenye Baraza la Mawaziri. Lowassa kutaka jambo hilo liende
mahakamani ni kwa kuwa ni kwenye mahakama ndiko kwa kuapa kiapo cha
kimahakama ndipo kiapo cha kutunza Siri za Baraza la Mawaziri hutenguka.
Leo Lowassa akithubutu kusema yale waliyojadiliana kwenye Baraza la
Mawaziri kuhusu Richmond atakuwa anafanya jinai inayofanana na uhaini.
Kama alivyosema Nape kwamba "Hawezi kusema kila kitu" ndivyo na Lowassa
naye anavyobanwa na kiapo cha uaminifu kwa Rais na Serikali ya Jamhuri
ya Muungano Tanzania.
Njia Pekee ya kukivunja Kiapo cha Waziri Mkuu alichokula Lowassa ni
kumpeleka Mahakamani ili huko akaseme ambayo akisema leo anaweza
kushitakiwa hata kwa Kosa la Uhaini! Kiapo hicho hakiwezi kutenguliwa
kwa Hoja ya Richmond kurudishwa Bungeni wala kwa Mwakyembe kujiapiza
kuachia uwaziri ili apambane kwenye majadiliano Bungeni,
Tags
Edward Lowassa
